Haya Museveni nae atangaza nia Uganda 2016

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Ikiwa leo tu rais wa Sudan Al Bashir ameondoka kirahisi Nchini Afrika ya Kusini baada ya kutobanwa na uongozi wa Serikali ya Nchi hiyo kinyume na amri ya ICC kuwa kiongozi huyo asitoke huko.

Saa hii BBC wanatangaza kauli ya Museveni Rais wa Uganda aliyeko madarakani kwa zaidi ya miaka 27 awaambia waganda angependa kura zao ifikapo mwaka 2016 katika uchaguzi mkuu.

Tayari mpinzani mkuu ameshatoa tamko kupinga uamuzi huo na tayari jeshi la polisi Uganda limeonya kuwepo kwa maandamano yeyote toka kwa upinzani kama fununu zinavyojieleza wao watapambana nao.

Hii ndiyo Afrika yetu na Ikulu zetu tamu nina wasiwasi wazungu watakuja tutenga baada ya muda kidogo, Mfano hai ni shida iliyopo Burundi na Nkurunziza kashindwa pewa ukweli wake na viongozi wetu afrika mashariki.

Pili ilisemekana na kagame nae atapenda kuendelea kuwepo kwenye kiti,rais wa Kongo DRC Kabila nae yupo tu kwenye kiti ingawa ameshapingwa sana atoke pale lakini wapi.

Ukienda kwa mzee wetu Mugabe yaleyale, Au wanashutumu ICC kua inaonea viongozi wa kiafrika je kwa picha ilivyo kwa viongozi wetu ni kweli wanaonewa?
 
Ni kweli viongozi wetu si wepesi wa kuacha madaraka lakini hili halijaanza leo, shida iliyopo ni nchi za magharibi na hila zao za kila namna kuhakikisha amani inatoweka ktk Mataifa kwa ajili ya maslahi yao
 
Acha kusingizia wazungu kila kitu
 
Kwani Kwini Elizabeth ametawala miaka mingapi vile? Tena anaenda mpaka Australia na New Zealand ambako waingereza waliopelekwa huko walikuwa majizi sugu huko kwao!!
 
shida sio kutawala je unakibalika na hauvunji sheria mlizokubaliana malkia hajawah kulalamikiwa hata siku moja hajavunja sheria uchumi uko vizuri njoo kwetu afrika mwendo wa kuvunja sheria hakuna jipya kwa nn tusilalamike
 
Ni kweli viongozi wetu si wepesi wa kuacha madaraka lakini hili halijaanza leo, shida iliyopo ni nchi za magharibi na hila zao za kila namna kuhakikisha amani inatoweka ktk Mataifa kwa ajili ya maslahi yao
kwa hiyo west ndiyo inawaambia wasiachie madaraka????
sio kila tatizo utafute wa kumsingizia, matatizo mengine ni sisi wasababishaji tuache kuitupia lawama west
 
wewe mburura sana....angalia powers na kwini na KINGI...hata israel ujeruman wana marais ila angalia powers walizopewa kwa katiba
 
Ni kweli viongozi wetu si wepesi wa kuacha madaraka lakini hili halijaanza leo, shida iliyopo ni nchi za magharibi na hila zao za kila namna kuhakikisha amani inatoweka ktk Mataifa kwa ajili ya maslahi yao

kwa level ya thinking ya sampuli ii africa kazi ni ndefu sana!!!! kila kitu tunasingizia wazungu ha ha ha baniani mbaya sio!!!

uongoz wa JF muweke thumb down symbol mtu aweze kuweka kuonyeshwa kuchukizwa na mawazo ya kipuuz kama sampuli ii
 
shida sio kutawala je unakibalika na hauvunji sheria mlizokubaliana malkia hajawah kulalamikiwa hata siku moja hajavunja sheria uchumi uko vizuri njoo kwetu afrika mwendo wa kuvunja sheria hakuna jipya kwa nn tusilalamike

Katiba inasemaje?hilo ndio muhimu.

Kama katiba haina limit basi hakuna tatizo kwa yeye kugombea.Nchi zinaongozwa kwa katiba.
 
kwa hiyo west ndiyo inawaambia wasiachie madaraka????
sio kila tatizo utafute wa kumsingizia, matatizo mengine ni sisi wasababishaji tuache kuitupia lawama west

Katiba katiba katiba

Angalia kwanza katiba yao kama ina term limit, kama haina basi hatuna hoja kwenye hili.
 
Kwa mtazamo huu wa wengine kutetea uovu ivunjaji sheria africa kazi bado nzito!labda wazungu waje watutengenezee chanjo ya kututoa ujinga,naangalia news hapa baada ya taifa stars kuboronga wengi wana suggest kocha atimuliwe kweli hilo ni suluhisho?kwanini hatutumii akili?tokea tanzania ianze kufukuza makocha ktk clubs na timu ya taifa nini kimebadilika?ndipo hapo nasema twahitaji chanjo!
 
Back
Top Bottom