Mwishoni mwa mwaka 2017 waziri wa fedha na mipango FILLIP MPANGO alitoa agizo la matumizi ya shilingi ya Tanzania katika huduma na ununuzi wa bidhaa kwa wananchi. Agizo hilo lilitegemewa kuanza kutekelezwa januari 1 mwaka huu.
Nimeyapata mazungumzo na Dr Kitojo Waitengere kutoka chuo kikuu cha kimataifa cha Diplomasia ambaye ameeleza nini chanzo cha kulega kwa utekelezaji wake pamoja na madhara yatakayojitokeza.