Pre GE2025 Haya ndio majina matatu ya wanachama wa CCM wanaoweza kupambana na Lissu jino kwa jino bandika bandua akimwaga mboga anamwaga ugali

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ni Mimi Kafulila au sijaelewa?

Hao wote niliowataja wamepambana na Lissu kwa hoja mara kadhaa nenda Kagoogle.
To me Kafulila is the best japo sio mwanasheria ila anajua siasa vizuri za Upinzani
 
Upo Sahihi Ndani Ya CCM Kwenyewe Hakuna Mwenye Jibu
 
Duh..
 
Kafulila sijui kwanini CCM haimtumii huyu jamaa nakumbuka wakati wa JPM alininyooshea balaa huyu mwehu
We una akili kama za mifugo! Nani mwehu? Angekuwa mwehu mngekuwa mnatafutana mwenye uwezo wa kujibu hoja zake na hamumpati? Kuanzia #1 hadi machawa wote mna haha tuu!
Usirudie tena kumwita mwehu, Bangladeshi!
 
Huna adabu

1]kabudi alishapingwa hajawahi jibu ,alipojibiwa kuhusu kubagazwa nchi ,lisu akasema kabudi anachamganya kati ya nchi na serikali

Kabudi ,uwakili alipewa wa heshima na hajawahi fault,ngumu lisu alifaulu

Polepole ,kwa lisu sisawa ,chamana hana labda aendelee kula maisha ya ubaloz
 
ongeza Makonda
 
Kwa Kafulila vipi mbona hujatoa comment orodha ni wanasiasa watatu
 
Hoja zingine kujibu kwake labda udanganye, ufanye manipulation au utishie.. otherwise kuna vitu havijibiki.... Hoja kama za Muungano Fatma karume angeweza kujibu vizuri ila hakuna chakujibu hapo.

Nakumbuka alivyoteuliwa Tulia Ackson kuwa naibu spika, Wabunge baadhi wakaibua hoja kuwa ameteuliwa kinyume na utaratibu. Tundu Lissu alikuwa bungeni na hakucomment chochote katika hilo (mi sielewi sana) lakini hiyo ilinipa kuelewa kuwa pengine kulikuwa na exceptions kwenye hilo na TL anaelewa hilo ndio maana aliwaacha watoa hoja wajivue nguo. Maana kisheria ingekuwa kinyume chake TL angekuwa wa kwanza kubeba bango.

Kuna hoja za kuunga mkono na kurekebisha, you can't win ukiamua kuzipinga, or else utawin kwa kumtisha mleta hoja, Dola inalijua hili vizuri.
 
Kwa upande wangu wana ccm waliomjulia Mh. Lisu ni hawa:-

1. Mh. Jakaya Kikwete
2. Mh. Hayati Samwel Sitta
3. Mh. Anna Makinda

Hawa tu nadhani hata Mh. Lisu anawahusudi linapokuja swala la demekrasia Tz.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…