Habari wana jamvi,
hapo mwanzo ilikua ni kitu kipya kuona serikali ikishindwa kuyatolea ufafanuzi masuala fulani yaliyojitokeza hapa nchini hadi kuitwa dhaifu.
Leo hii hadi taasisi zake zimefuata huo utaratibu au mfumo usio rasmi. Inashangaza sana kwa taasisi tena za elimu ya juu TCU/NACTE kushindwa kutolea ufafanuzi wa mkanganyiko katika suala la selection, hapo mwanzo waliwajuza vijana wetu kuwa wangewatolea hizo post tarehe 22/10 ila hadi sasa ni hali ya sintofahamu ikiendelea maana ni vyuo tena baadhi tu vimetoa hizo post.
Vijana wamebaki hawajua nini kinafuata hasa baada ya TCU kutoa tangazo la TRANSFER na utaratibu wake wakati zaidi ya 60% hawajua either wamechaguliwa chuo gani au hawajachaguliwa. Hali sio shwari hasa ukitembelea ukurasa wa NACTE facebook vijana wanaonyesha hali ya kuchoshwa na kukata tamaa.
Wengi wao wakijiuliza nini tatizo kwani waliaminishwa CAS ni mfumo mzuri na rahisi kudahili ila kwa hali ya sasa wanamashaka na hilo baada ya kujitokeza pia kwa Multiple selections.
TCU/NACTE tafadhalini kuweni japo professionals na mfano kwa taasisi zingine. Wapeni vijana taarifa rasmi wajue nini kinaendelea.
Ahsanteni.