Haya ndio mazungumzo ya Watanzania eti?

zagarinojo

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2020
Posts
2,622
Reaction score
2,846
Kuna jamaa eti ameniambia asilimia za maongezi ya watanzania ziko hivi.

1.Siasa wanaziongelea asilimia 30%
2.Mpira wanauongelea asilimia 50%
3.Muziki na Burudani asilimia 20%
4.Babes na magashi asilimia 10%

Mambo ya msingi na kujenga taifa asilima 000.001%
 
Matunda ya Miaka 43 ya Utawala wa CCM Maradhi, Ujinga na Umaskini wa kutupwa. Walau wakati wa TANU hawajamaa walikuwa wanakondeana, tangu CCM ifanye Azimio la Zanzibar 1992, kasi ya unono na ukibonge inaongezea maradufu!
 
Ila asilimia wabongo tulikalilishwa lazima iwe mwisho 100%huwa zinavuka wakati mwingine
Kwa scenario yako hapo juu haiwezekani kuvuka 100%.

100% inaweza kuvukwa kama malengo/kiwango/makadirio nk uliyoweka awali yamevukwa, mfano ulitarajia kwa mwezi kukusanya mapato ya Tzs 1000 then ukakusanya Tzs 1400 kwa mwezi husika, hapo utasema nimekusanya mapato kwa 140%. Yaani umevuka malengo kwa 40%.
 
Bora umemuelewesha. Hisabati ni ngumu sana.
 
Ila asilimia wabongo tulikalilishwa lazima iwe mwisho 100%huwa zinavuka wakati mwingine
Wewe ndio umekariri. Inaonekana uelewa wako ni mdogo sana. Nasema hivi kupitia uzi wako na comments zako pia.
 
Ila asilimia wabongo tulikalilishwa lazima iwe mwisho 100%huwa zinavuka wakati mwingine
Dah.....Dogo.......asilimia ni namba ambayo iko chini 100....ni namba ambayo inaonesha kiasi cha kitu kutoka katika kitu kizima...mfano ukigawa chungwa kwa watu wawili kila mmoja atapata nusu..1/2...yaani 50% ambayo ni 50/100...
Mfano mwaka huu inakadiriwa Magufuli atapata kura zaidi ya 80%.....maana yake 20% ya kura ndiyo watagawana wagombea wengine......lakini kamwe haiwezekani kama Magufuli kapata 80%...halafu tena Lissu akapata 99%...naye Profesa akapata 98%......
Nashauri....... hisabati ni muhimu sana kuliko kiingereza 🤭
 
Nakataa mambo ya msingi ya kujenga taifa, asilimia umeifukua wapi? Tungeingiaje uchumi wa kati?
 

TCRA kuna kafiri huku kamwaga data za Uongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…