Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363

Kamati ya Maridhiano Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake, Mhe. Hassan Nassor Moyo, imefafanua
MAMLAKA KAMILI inayotaka Zanzibar iyasimamie yenyewe ambayo yanajumuisha mambo
yafuatayo:
1. Mipaka ya Zanzibar kama ilivyokuwa kabla ya tarehe 26 Aprili, 1964.
2. Uraia.
3. Uhamiaji.
4. Mambo ya Nje.
5. Polisi.
6. Sarafu, Mabenki na Usimamizi wa Fedha za Kigeni.
7. Mikopo na Biashara ya Nchi za Nje.
8. Kodi ya Mapato, Ushuru wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa.
9. Bandari, Usafiri wa Anga, Posta na Simu.
10. Leseni ya Viwanda na Takwimu.
11. Elimu ya Juu.
12. Maliasili ya mafuta na gesi asilia na maliasili nyengine zote zilizomo ardhini na baharini.
13. Baraza la Taifa la Mitihani.
14. Usafiri na Usafirishaji wa Anga.
15. Utafiti.
16. Takwimu.
17. Vyama vya Siasa.
Ukiondoa hayo yale maeneo mengine yaliyopendekezwa kubaki katika Muungano basi Kamati
imetaka utaratibu wa uendeshaji na usimamizi wake uwe wa wazi na uhusishe na ushirikishe
pande zote mbili kwa usawa kama nchi washirika - Zanzibar na Tanganyika.
CHANZO. http://zanzibarniitakayo.blogspot.com/2013/05/mapendekezo-ya-kamati-ya-maridhiano.html