EllySkyWilly
JF-Expert Member
- Aug 28, 2020
- 2,204
- 2,085
Haya ndio yale tunayosema "utumwa maomboleo" angalia tulijifunza kuwa kilimo cha chai kipo Sri Lanka lakin ukienda pale mufindi iringa unakuta wahehe,wabena,wakinga wanalima chai,tukasoma kuwa kilimo cha mahindi kipo Marekani hatukuambiwa kuwa mikoa ya nyanda za juu kusini yote wanalima mahindi,tena ya kulisha sio tu Tanzania bali hata mataifa jiran.
Tukasoma ngano wanalima Burma lakini pale Makete wanalima ngano ya kufa mtu,ngano ya makete ukila na ile mikate ya Kikinga usipimie.Wakasema Cuba ndio walimaji wa miwa lakin pale Morogoro,Kagera na Arusha wanalima miwa ambayo tunaweza tukazalisha sukari yetu ya ndani na ikafaa kwa matumizi yetu ya ndani na pesa ikawa kwenye mzunguko palepale.
Wakasema Pamba inalimwa India,lakin nenda Shinyanga,Mwanza na mikoa ya zone ya kaskazini,pamba kila sehemu, wakasema ndizi inalimwa Jamaica,njoo kagera,Kilimanjaro,Mbeya ndizi zinalimwa usipimie,mpaka masoko tunakosa.Upasuaji wa mbao wanasema Canada pita pale iringa utaona shughuli za kiuchumi za kupasua mbao,njoo mpaka makete utakuta mashamba ya miti na shughuli za kupasua mbao kila kata.
Wanasema ufugaji ng'ombe ni Dernmak well,njoo kwa jamii ya wamasai,wasukuma yaani mikoa ya mwanza,arusha,shinyanga,Dodoma, ng'ombe wapo kila sehemu..wanasema Uvuvi wa Samaki upo Norway lakin Tanzania ina maziwa makuu matatu makubwa,Tanganyika ziwa lenye kina kirefu Afrika, Victoria na nyasa,njoo maziwa ya ndani yapo mengine matatu makubwa njoo na bahari ya hindi yote ipo sehemu ya Tanzania,uvuvi watasemaje Norway inaongoza? 2011 meli kubwa ilikamatwa samaki zetu wakitoroshwa halafu wanasema norway? Uchimbaji mafuta wanasema Kuwait, well,sisi gesi tunayo Sitaki kujua wachina waliingiaje lakin uwezo wa kusambaza na kutumia gesi yetu tunao.
Hiyo namba 21 tulijifunza juu ya biashara ya usafirishwaji duniani,tulisoma juu ya mijndombinu mizuri ulaya,treni za umeme,meli kubwa za biashara,mandege ya biashara na Barabara nzuri,asante Mungu, tupo hapo sasa ukilinganisha na tulipotoka ATCL imefufuliwa,treni ya umeme inajengwa,barabara zinajengwa kazi nzuri ya rais Magufuli na CCM.
Nini namaanisha? Tulipoteza muda mwingi kusoma mambo ambayo hayana mahusiano ya moja kwa moja na mazingira ya taifa letu,mambo ambayo yalijenga mentality ya kudharau vya kwetu na kuona vya ulaya na Marekani ni vizuri.Sijafanya vizuri sijafanya tafiti sijui kama bado haya mambo yanafundishwa mashuleni au la, lakin sasa ipo haja ya kubadili historia kutoka kujifunza mambo ambayo hayana tija kwetu tukasoma mambo ambayo hata tukijifunza na changamoto zake basi tutatatua chanbamoto hizo kwa namna mazingira yetu yanavyotufanya tuwe.
Mfano mzuri, Jamaica hajui kama Tanzania tunalima ndizi pale kwa wachaga au wanhakyusa au wahaya lakin sisi tunalazimishwa kujua wanachofanya Jamaica, wanachofanya Marekani,wanachofanya Canada nk,ndio maana leo kijana aliyejifunza hayo miaka 20,30,40 nyuma hawezi kuamin kuwa ndizi za mbeya, lagers, moshi ni nzuri zaidi ya zile za kwenye fridge zinazotoka Jamaica.Huyo hata ukimwambia kuwa Tanzania tunauwezo wa ku deal na virus vidogo vya corona na yukavimaliza kwa tiba zetu hawezi akaamini kwasababu alijifunza kuwa India,USA,Cuba ndo wanaotoa tiba peke nzuri duniani.
Ndio yaleyale ya kusoma kilasiku historia ya(Tanganyika alitawaliwa na mwingereza) mwingereza akajenga reli,barabara,shule,umeme,akajenga ikulu,akajenga mfumo wa uongozi,akatuachia mfumo wa katiba nk,halafu leo aone rais Magufuli anawajibu hao waingereza kuwa tutaongoza nchi kwa namna tunavyo fafanua mambo yetu kama taifa huru, haki hawezi akaelewa kwasababu akili yake inaamini mambo ya tawala lazima ukope akili kutoka kwa Marekani au uingereza, ataamini kuwa akija Tanzania Obama au Bush au Biden basi ndo fahari lakin rais Magufuli asipotoka hapa akaenda huko mentality za utumwa wa mikopo inajaa kichwani.
Ipo haja ya kusoma yale yanayotuhusu,nimeona BBC leo inasema siku ya mapinduzi na wakasema timjue sultan wa mwisho aliyetawala Zanzibar inatuhusu nini sisi? Sultan wa Zanzibar anatuhusu nini sisi? Tunahitaj kujua mapinduzi ya kisiasa,kiuchumi na kijamii yaliyofanywa na serikali huru ya wana wa nyumbani katika kujiletea ukombozi wao, kazi waliyofanya akina mzee Karume, Mwinyi nk ni kubwa,hao ma sultan walitugawa law rangi zetu, uchumi wetu, leo pale watu wote wanapata huduma sawa za kijamii bila kuangalia rangi zao nk..haya ndio ya msingi ya kujifunza,lakin kwasababu hata hao BBC swahili ni wakala wa ubeberu hatushangai.
Naheshimu sana kazi za kizalendo anazofanya JPM,japo wengine bado si wazalendo imagine miwa tunalima hapa hapa nyumbani lakin sukari inaweza kupanda bei usiipate,alizeti inalimwa pale Kigoma lakin mafuta yakawa adimu kwasababu watu wanamaslah yao binafsi,kwann mtupe milolongo ya mambo wakati vitu ni vyetu?
Tupo tayari kutumia kwa tabaka la level zetu,msitutafutie sababu za mara ooh ziwe first class kama za ulaya wakati wanunuzi sisi uwezo wetu ni hizo mnazosema residual mtupe na tuzalishe law kadri ya uwezo wa manunuzi ya watu wetu..itoshe kusema kuwa utumwa wa kifikra kupitia mifumo ya elimu isiyoshahabiana na mazingira halisi ya nyumbani bado ni muendelezo wa ukoloni maomboleo na tunahihaji kuupiga vita mifumo hiyo.