Haya ndio...

Nguvu moja

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2017
Posts
3,371
Reaction score
2,713
Madhara ya kujichubua


Katika baadhi ya sehemu duniani watu wanaamini kuwa ngozi angavu huashiria uzuri, utajiri na uwezo(kifedha) alionao mtu.Katika baadhi ya sehemu watu wenye ngozi nyeusi huchukuliwa kuwa wapo chini ya kiwango,

hii hupelekea watu hawa kutumia ving´arisha ngozi kama krimu, vidonge au nyenzo zingine kubadilisha ngozi zao.

Tafiti zinaonyesha kwamba wavulana na wasichana hupendelea kutumia bidhaa zinazong´arisha ngozi ili waweze kupata hadhi nzuri katika kundi la familia zao, na jamii. Kwa kweli,hata matangazo yanayoonyeshwa kwenye televisheni mbalimbali huonyesha kitu hiki. Mambo hayo yote huwa na athari kubwa juu ya mawazo ya vijana wa kiume na wakike ambayo hupelekea kuwafanya wachague chochote wanachomudu kati ya krimu au vidonge.

Madhara ya kujichubua ni yapi?
Mtu anaeyejichubua anaweza kupata kansa ya ngozi, chunusi, uvimbe katika ngozi, ngozi kuwa nyembamba,Kuongezeka kwa hamu ya kula na uzito,kutokwa na mabaka, pumu, kupata watoto wenye kasoro, kupata matatizo ya akili, kuharibika kwa ini, kuharibika kwa mishipa ya fahamu pamoja na figo kutokana na kiwango kikubwa cha zebaki(mercury) kilichomo katika krimu,Osteoporosis(kupungua kwa uzito wa mifupa ambapo huongeza hatari ya kuvunjika kwa mifupa)

Baadhi ya madhara haya huonekaa mara moja na mengine hujitokeza kadri mtu anavyotumia ving´arisha ngozi.

 
Nyuma ya dereva.....ngoja waje
 
Mtu akijichubua anatoka kwenye uhalisia wa rangi yake na kuwa mwekundu.

Ukikutana nae Basi anatia kinyaa
Mimi kwa kweli Bora nipambane na rangi yangu ,i am proud of it,i love my black color

.huko mbeleni weusi tutabaki wa kuhesabika Kama sio pekeyangu[emoji28]

Ila acha tupungue jamani tubaki wachache,siku iz Kila mtu mweupe usoni mkononi mweusi,mashavu mekundu..Ana mchanganyiko wa rangi Kama kachumbari [emoji1787]
 
Yangu mafuta ni baby Jonthon na baby care....zawad Zanzibar czion cku hiz😜 izo krim nawaachiaga wamama&wanaume wa Dar😯
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…