Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
- Thread starter
-
- #21
Shimo kubwa ambalo lililopo katika barabara ya Morogoro karibu na NSSF jijini Dar es Salaam. (Picha na Hamisi Athumani)
My Take:
Kwa aliye kwenye Benz ameendelea sana; kwa anayetembea kwa miguu anaona maendeleo ya mwenye Benz na kuyatamani. Kwa mhandisi wa barabara, na yeye anatamani kuwa na Benz na viongozi wa Halmashauri wanajiuliza ni jinsi gani wataweza kuagiza Benz kwa watendaji wake.
Barabara mara nyingi uharibika kipindi cha masika, na wengi wetu tumeona jinsi gani masika ya Bongo mwaka huu ilivyokuwa... zaidi kuna wizi wa vyuma vya mifuniko ya misingi ya maji taka...
Kipi bora? Kutengeneza barabara hiyo au kununua magari mazuri ya kutufanya tujisikie vizuri?
Mkuu! Ukiangalia kwa haraka haraka kune mengine kama matatu ambayo yako mbioni kugeuka mahandaki! Nayo yanasubiri masika ijayo................
Ukiacha wizi wa mifuniko, mahandaki aka mashimo kwenye barabara za mijini huchangiwa sana na mvua hii inatokea hata kwenye nchi zilizoendelea, Tumewahi kujadili kwa kina hapa JF juu ya matatizo ya misingi ya maji taka na nina hakika yale tuliojadili yanaweza kutoa suluhisho katika picha hii...
Aidha MKJJ amefanya unazi mkubwa kwa kuweka picha hiyo na kuzungumzia maendeleo, ilhali mvua haina msalie hata kama una maendeleo ya aina gani...
Pengine kilichokosekana hapo ni alama za tahadhali kwa wenye magari na watembeao kwa miguu.
Nimekupata vizuri sana, Sikua na lengo la kutetea uzembe ila nilikuwa najaribu kuangalia ni nini chanzo cha tatizo hilo, kwani mada yenyewe imekuja kwa namna ya kejeli na ikaendelea kuchangiwa katika mitiririko wa kejeli.Kibunango wa Tampere! Huko kwenu si kuna snow kibao? Umewahi kuwasikia wenyewe wakisingizia snow kwa ajili ya matatizo yao? Mvua inajulikana, na wanao'design' hizi barabara wanatakiwa watilie hilo maanani (kuna kitu kinaitwa storm water drainage). Hapa ni uzembe, period. Uzembe wa kutosafisha hizo drains. uzembe wa kutochukua hatua mara tatizo linapojitokeza. Hilo shimo si saizi ya mfuniko.....
Amandla!
Kibunango wa Tampere! Huko kwenu si kuna snow kibao? Umewahi kuwasikia wenyewe wakisingizia snow kwa ajili ya matatizo yao? Mvua inajulikana, na wanao'design' hizi barabara wanatakiwa watilie hilo maanani (kuna kitu kinaitwa storm water drainage). Hapa ni uzembe, period. Uzembe wa kutosafisha hizo drains. uzembe wa kutochukua hatua mara tatizo linapojitokeza. Hilo shimo si saizi ya mfuniko. Mfuniko umeibwa, wakaangalia. Mvua ya kwanza ikaja na ikapanua shimo, wanaangalia! Mvuo ya pili imekuja na kupanua shimo zaidi, wanaangalia! Mpaka siku ambapo gari la mkubwa litakapodumbukia ndipo watakimbia kwa hao walio kwenye hilo benzi kuomba ufadhili wa kutengeneza barabara UPYA maana imeharibika beyond repair! Wizi najua upo lakini kwa nini wasitafute solution ( vifuniko vya zege, kuweka lock kwenye vifuniko ambazo si rahisi kuvunja n.k) ya hilo badala ya kungoja mtu aje apoteze maisha kwenye haya makorongo? Hapa, Mkuu hamna cha kujitetea. Ni dalili ya matatizo tuliyonayo na jawabu ni kutafuta namna ya kutoka hapa tulipo.
Amandla!
Nimekupata vizuri sana, Sikua na lengo la kutetea uzembe ila nilikuwa najaribu kuangalia ni nini chanzo cha tatizo hilo, kwani mada yenyewe imekuja kwa namna ya kejeli na ikaendelea kuchangiwa katika mitiririko wa kejeli.
Hilo la mifuniko ya vyuma ni bora asasi husika zikawazinafuatilia wale wauzaji na wayeyushaji wa vyuma chakavu kwani ndipo upelekwa huko na hao wezi.
tatizo si mvua bwana, kama kungekuwa na miundombinu dhabiti tusingeyapata haya, hebu piteni barabara ya Nyerere pindi mvua inaponyesha, ni aibu drainage system mbovu, inapeleka maji taratibu sana hivyo haiwezi kuhimili mvua hata kidogo tu, ni mto unageuka pale kama siyo ziwa kabisa, ngoja siku wapate aibu ya kuogelea na washaipata naona wameanza kuchimba chimba mitaro, manake ile barabara si ndiyo ya kuelekea majuu, just imagine siku hao wageni wao wa sullivan wakianza kuwasili waogelee kwenye maji ya kinyesi.
Dar es Salaam panakatisha tamaa sana, watu wanajenga majumba ya kifahari, wananunua na magari ya kifahari, ila miundombinu ni zero kabisa! Hakuna drainage system, barabara siku hizi zinajengwa kwa kulipuliwa tu, haiishi hata miaka miwili tayari zinakuwa na mashimo, mfano ni barabara ya kwenda Tabata na Segerea. Pia kuna barabara moja inapita mtaa wa Ursino, kwenye nyumba binafsi ya Kikwete, imewekwa lami mara baada ya Mheshimiwa kuingia madarakani, lakini tayari ina shimo!!!! Hiyo ni mifano michache tu.
Katikati ya jiji ni balaa, hakuan......................!
Ningefurahi zaidi kama ningeona plate number nijue kama ni TZ au Vipi?
Lakini shimo linaonyesha siyo bongo maana walau wakati wa mafuriko maji yangekuwa hayajaii.
Na kama ni ki "assume" ni bongo, naona tatizo sio tofauti ya gari na barabara ila tofauti ya fikra sahihi na utekelezaji wake.