Haya ndiyo magereza manne ya kifahari zaidi duniani

Haya ndiyo magereza manne ya kifahari zaidi duniani

Hemedy Jr Junior

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2023
Posts
915
Reaction score
1,082
images (11).jpeg

LIPO AMBALO WAFUNGWA WANALIPWA Tsh. 18,000 NA LINGINE UKIINGIA UNALIPIA ADA KILA MWISHO WA MWEZI.

1. ARANJUEZ,Gereza hili linapatikana huko Hispania Jijini Madrid. Inaaminika hili ndio Gereza la kifahari na la kitofauti zaidi duniani,kwani wafungwa wa hili gereza huishi maisha kifahari sana, kwenye hili gereza kama mfungwa ana mtoto mdogo anaruhusiwa kukaa naye mpaka pale atakapotimiza mwaka mmoja,hufanya hivi ili mtoto apate malezi ya wazazi wote. Pia gereza hili huruhusu wazazi hao wakae pamoja yaani baba na mama wa mtoto ili kuimarisha malezi bora ya mtoto.

2. SANTA ANA. Gereza hili lipo nchini Marekani,Jela hili liko kitofauti sana,Wanaokaa jela hii ni wenye uwezo wa kifedha tuu,jela hii unapofika tuu itabidi ulipie dola za kimarekani $136 ili upate kusajiliwa rasmi kama mfungwa wa jela hii. Pia kwa siku ada yake ni takribani dola $108, yaani ulipe kiasi hicho cha fedha kila siku.

Na cha tofauti kingine ni kwamba askari magereza hawarusiwi kuwaita wafungwa wa humo "Mfungwa",huwa wanaitwa Wageni.

3. BASTOY, Gereza hili lipo Norway kwenye kisiwa cha Bastoy. Gereza hili n kubwa lakini linachukuwa takribani wafungwa 100 tuu hii n kwa sababu ya kuepusha msongano wa watu,lakini pia wafungwa wa humu huishi maisha ya kifahari kama kucheza tenesi,kuotea jua na kupanda farasi.

Pia kwenye upande wa chakula gereza humpatia kila mfungwa na kama hajakipenda chakula hicho basi hununuliwa na hujipikia mwenyewe. Pia kila mfungwa hupewa marupurupu ya dola $90 kila mwezi pia hulipwa dola $8 kama mshahara wao kwa siku hii ni kwa ajili ya kazi za kila siku wazifanyazo huko jela.

Unaweza sema wanafanyiwa kutokana na makosa madogo hapana, Bastoy wapo watu wameua,wamebaka pia. Yote haya hufanywa kutokana na serikali ya Norway huamini kuwa uhuru na furaha ya mtu ni muhimu zaidi.

4 .QINCHENG, Gereza hili linapatikana nchini China,Gereza hili hapo mwanzoni lilikuwa ni spesho kwa ajili ya wafungwa wa kivita, lakini hapo mbeleni lilibadilishwa na kuwa gereza rasmi kwa ajili ya wanasiasa wakubwa na watu wenye wadhifa wa juu nchini humo, Selo za wafungwa kuna kila huduma unayoipata kwenye Hoteli. Imeandaliwa na Hemedy jr Junior
 
Msidanganyike.

Sehemu yoyote inayolindwa na BUNDUKI na binadamu kanyimwa UHURU maana yake haina usalama

Gereza namba 2 alilotaja mleta mada ni hilo, hapo ni mwaka 2019
Screenshot_20230221-224934.png
 
Back
Top Bottom