Hiyo slogan ya Maisha bora kwa kila Mtanzania haitoki tena kinywani mwa Kikwete! Bila shaka ameona mabanda yanayohifadhi washabiki wake; ameona watoto wa Kitanzania wakitoka kamasi , vifua nje na "vitambi" vya utapia mlo. Fikiria thamani ya nyumba hiyo ukilinganisha na thamani ya picha iliyobandikwa ukutani! Na ukweli ni kwamba nyumba hiyo pichani ni bora kuliko hata baadhi ya vibanda vilivyoko polini jimboni kwa Kikwete. Jee wewe mwana JF ungekuwa Kikwete ungetamka tena Maisha bora kwa kila Mtz? Machozi yananilengalenga... Dr Slaa ukiingia Ikulu wakumbuke sana watu maskini ili uurithi ufalme wa Mungu.