Flora Mbasha Afunguka Mazito Mpaka Mengine
Hayawezi Elezeka Kuhusu Mumewe Mbasha, Ni
Hatari Sana
Nimefikia uamuzi wa kudai talaka kutokana na
kuchoshwa na vitendo vya ukatili nilivyokuwa
nafanyiwa na mume wangu, kwa zaidi ya miaka8
na hata sasa bado anaendeleaje, Kwani hata
kuongea uongo kwenye media juu yangu ni
ukatili pia.. nimekuwa nikinyanyaswa kijinsia na
mume wangu na sikuwahi kutoa taarifa mahala
popote kutokana na vitisho alivyokuwa
akinitisha.
Watu Wengi wanafikiri nilikuwa na ndoa nzuri
sana lakini kumbe nilikuwa Nikivumilia tu Kwani
niliamini ipo siku atabadilika maana nilimpenda
sana mume wangu.Nilijaribu kuficha huzuni na
maumivu yangu kila nilipotoka na mume wangu
kwenda kwenye Huduma au mahala pengine penye
mkusanyiko wa watu.
Sijawahi hata Mara moja kutoa taarifa hata kwa
wazazi wangu juu ukatili niliokuwa nafanyiwa na
mume wangu.Kwanza sikutaka kumvunjia heshima
kwa ndugu zangu na pia alikuwa akinitishia
kuniua na kuongeza kunifanyia ukatili huo.
Kutokana na historia yake ya nyuma alikuwa na
uwezo wa kunifanya chochote na ndiyo maana
nilikuwa nikimwogopa sana.
Siku zote nilikuwa akilala na panga kitandani
ambalo ndilo alikuwa akinipiga nalo na kuapa
kunichana chana Mwili Kabla ya kuniua.
Kipigo hicho nimekuwa nikikipata hata
ninapokuwa kwenye Huduma bila kujali natakiwa
kuwa kwenye mood nzuri ili ni perfome vizuri.
Nimevumilia muda mrefu lakini ndo mateso
yakawa yanazidi na kufikia hatua ya kufukuzwa
akidai yeye ana mwanamke mwingine wa dini yake
ya zamani hivyo anataka amlete hapo nyumbani.
Nilikataa kuondoka na kumwambia amlete tu,
tutaishi wote mimi nitakuwa nikilala chini maana
nshazoea siku zote Amekuwa akinilaza
chini ,alivyoona siku zinazidi kwenda na mimi
nimegoma kuondoka basi akaamua sasa isiwe siri
ya chumbani tena Akawa ananitoa ananipigia
sebuleni na anasema nataka mtoto na wengine
wote wajue kuwa huwa nakupiga humu
ndani.Ikafika hatua anataka kunitoa nje ya geti
ili majirani wajue kuwa huwa napigwa na
anifukuze mbele yao.
Kwa Miaka yote alinizuia kufungua account bank
na kudai kuwa yeye ndo mwanaume hivyo pesa
zote ataweka yeye. So pesa zangu zote
nilizokuwa naingiza alikuwa akichukuwa yeye na
kuzihifadhi kwa account yake binafsi.
Sikuwa nikibaki hata na mia.Nilijaribu kufanya
biashara lakini napo pesa zote akawa akichukuwa
yeye ikabidi niache.. Nikitaka hata vocha ya mia
tano Lazima nimwombe hela na niitolee maelezo
ninampigia nani.
Mume wangu kwa kipindi chote hakuwahi kuwa na
kazi yoyote zaidi ya kunifanya mimi ndo biashara
yake. Lengo lake ilikuwa ni kunitumia mimi kwa
maslahi yake na sio upendo kama mke wake.
Hakuwahi kunipenda hata yeye mwenyewe hukiri
kuwa alinioa tu basi ili afanikiwe kwenda ulaya
kwa kuwa mimi nilikuwa nikisafiri na babu yangu.
Na yeye kila akijaribu kwenda nje anashindwa.
Kuna mambo mengi ya ukatili aliyokuwa
akiyafanya ndani siwezi kuyasema kwa ajili ya
maadili na pia bado Ninamheshimu kama mzazi
mwenzangu. Alipoona siondoki pamoja na vipigo,
matusi na kunifukuza kote.
Akasema nitahakikisha nakufanyia jambo ambalo
utaondoka mwenyewe humu ndani bila kupenda
sitaki kuzungumzia suala ambalo liko mahakani
ingawa hilo nahisindilo alilokuwa kadhamiria ili tu
niondoke.
Nilijaribu sana kumsihi tukae kikao na wazee ili
watushauri na kutusaidia lakini nilikuwa
nikiambulia matusi tu ya nguoni ambayo siwezi
kuyaandika hapa.
Siku niliyoondoka nyumbani alidhamiria kuniua
alidai hata akiniuà hakuna atakaye amini kuwa ni
yeye kaniua, na ni kweli maana sikuwahi kushtaki
mahala popote.
Alichukuwa panga akanipiga nalo kisha akaniniga
hadi nikaishiwa nguvu .Aliponiachia sielewi
nilitokaje ndani. Ugomvi mkubwa ulitokana na
mimi kukataa kufanya tenda la ndoa kinyume na
maumbile.
Amekuwa Alinipiga na kunilazimisha kufanya
tenda hilo kinyume na maumbike kwa miaka mingi
lakini nikisema bora nife kuliko kutendewa
ukatili huo.Amekuwa akidai kuwa wanawake
tumeumbwa ili tufanyiwe tenda hilo la ndoa mbele
na nyuma so ni haki yake.
Niliondoka kwake nikiwa na sh elfu mbili tu.
Nilimwachia kila kitu nyumba gari na pesa zote
zikiwa kwa account yake zaidi ya milioni
50.Sikuwa na uwezo wa kutoa pesa maana ni
account yake binafsi.
Nimejitahidi sana kumwita kwenye vikao hata vya
familia ili tu tujaribu kuzungum za lakini
amekuwa akionesha dharau tu na kusema yeye
haitaji ndoa tena anaoa mke mwingine hivyo
hawezi kusuluhishwa.
Ingawa Amekuwa akidanganya sana kwenye
media. Nilimwuliza Unapata faida gani
unapodanganya watu kuhusu mimi?
Akasema yeye amechafuka kwa ubakaji so acha
na mimi nichafuke na akasema atahakikisha
sifanyi huduma sehemu yoyote labda nihame nchi.
Kama msg hizo angekuwa amezituma bila
kuandika na matusi ningezikopi but zaidi kauli
zake ni za matusi. Hivyo imefika mahali nimeona
bora tuachane kisheria na pia nipate haki yangu
maana mume wangu anajivunia mali ambazo
hakuzitolea jasho yeye na huku anawatapeli
watu kwa kudai kuwa hana pesa maana mimi
nimeondoka nazo wakati ni uongo mtupu.
Mimi ninapanda daladala siku hizi sababu sina
uwezo wa kuwa na gari hadi niazime kwa
marafiki zangu. Mume wangu amekataa hata
kumsomesha mtoto sasa hivi nahangaika kutafuta
ada ili mtoto arudi shule lakini pesa yote anayo
anayo Mbasha.
Sasa sijui hapo ananikomesha mimi au mwanaye.!
maana urithi wa mtoto ni elimu bora na mzazi
anayempenda mwanaye atapambana ili
kuhakikisha mtoto anapata elimu bora.
Nilikaa kimya muda mrefu sikutaka kuzungumza
lakini imefika mahali Nimechoka maana huyu
bwana hajiheshimu. Tukikutana anasema sio yeye
anayepeleka habari mitandaoni.
Ninaomba wanaume wenyewe Mfano wake waache
kuwafanyia ukatili wake zao majumbani.Najua
wako Wengi sana wanao nyanyasika kama ilivyo
kuwa kwangu lakini Hawana sehemu za kukimbilia
Hivyo wanavumilia tu na mwisho wa siku
wanakufa na kuacha watoto wakiteseka.
Mimi Nilivumilia zaidi ya Miaka 8 lakini imefika
mahali enough is enough. Maandiko matakatifu
yanasema, ndoa haivunjwi isipokuwa kwa
uasherati.
Acha nife kwa mapenzi ya Mungu na sio kwa
mapenzi ya mtu..Na ni naamini sitakufa mpaka
ndoto zangu zitimie.
Mume wangu ameapa kuwa atahakikisha sifanyi
Huduma tena lakini ninasema katika Jina la
YESU, kama Bwana aishivyo, mwanzilishi wa
huduma yangu ni Mungu Hivyo mmalizaji wa
Huduma yangu ni Mungu mwenyewe.
Na sasa ninajipanga kumwimbia Mungu kama
sitaimba tena.Wakati mwingine usipokuwa
mwangalifu ndoa inaweza kukukosesha ufalme
wa mbinguni hasa Ukiingia kwenye ndoa isiyo
sahihi. Ninampenda sana mume wangu lakini
ninampenda Mungu wangu zaidi. Ahsante.
Nimeamua kuandika Maana Nimechoka kuficha
maovu aliyokuwa akinitendea.Nimemtunzia
heshima muda wote maana sikutaka jamii imjue ni
mtu wa aina gani but yeye anatumia ukimya
wangu kama udhaifu so naona bora niweze wazi
ili jamii imtambue mimi yamenikuta najua Wapo
Wengi tu wanapitia mateso niliyoyapitia mimi.
Kutokana na vitisho wanaendelea kunyanyaswa.
That is not fair kwa kweli.Mimi ningekufa Kabla
ya wakati wangu lakini namshukuru Mungu niko
hao hata sasa na pia ili kuwaonya wanaume
wanaume wenyewe tabia kama yake.
Kama umemshoka mwanamke achaneni kwa amani
sio kumnyanyasa mwanamke kama alivyokuwa
anafanya Mbasha kwangu.
Ninapinga vikali unyanyasaji wa wanawake na
watoto majumbani.
haya ndo kasema flora mbasha si mimi