Nikifa MkeWangu Asiolewe
JF-Expert Member
- Feb 26, 2024
- 6,944
- 14,351
Ni maoni yangu yanastahili kupingwa,kuungwa mkono au kukosolewa ama kuboresha zaidi.
Kwa mwanaume jambo ambalo unapaswa kulipa kipaumbele zaidi unapoanza maisha Yako ya kujitegemea boresha kwanza sehemu ya kulala.
Kwanini napendekeza sehemu ya kulala iwe nzuri.
Baada ya michakato,kazi ngumu na harakati za hapa na pale za kutwa nzima sehemu pekee ya kutuliza akili na uchovu ni kitandani unapolala uwe umeoa au hujaoa.
•Ni sehemu pekee ambayo mwili na akili hupumzika na kuchakata vilivyo ukiwa umetulia.
Kitandani ni sehemu pekee ambayo binadamu hunitumia kupumzika Kwa muda mrefu zaidi kuliko sehemu yoyote Ile.
Unapolala sehemu nzuri hata mwili wako utaamka ukiwa na nguvu tele.
•Ni sehemu pekee ya kuiwaza kesho Yako.
Ukweli usiopingika ukiwa kitandani baada ya kupigika na kazi za hapa na pale ni muda Sasa wa kupumzika na kutafakari zaidi maisha Yako ya badae.
Siyo rahisi sana kupata muda wa kutafakari kama hata sehemu ya kulala unaiwaza yaani wewe mwenyewe huipendi mara nyingi utakuwa unachelewa hata kurudi kwako Ili masaa yaende ukija kujitupia kitandani baasi ni kulala Moja Kwa Moja Kwa sababu umekuja Kwa kuchelewa.
•Hata Girlfriend wako atakuthamini zaidi kama wewe mwenyewe umejipa thamani kupitia kitanda chako.
Kataa ukubali wanawake wengi wanapenda usafi na unadhifu hasa sehemu unayolala haijarishi unalala chini ama juu lakini ukweli ni kwamba unapaswa upaboreshe zaidi pawe pazuri.
Hii haijarishi uwezo wako hata kama una godoro la Inchi4 ninachosema ni usafi na umaridadi wako.
Sisi tuliozaliwa kwenye familia za kifugaji tunajua maana halisi ya kulala pazuri
Nimelala kwenye ngozi ya ng'ombe Hadi natumiza miaka 13.
Nikaanza kulalia godoro la pamba Kwa Sasa wanaita msabato na wanaweka vitambaa hasa mabaki ya kwenye cherehani.
Siku nilipo anza kulala pazuri niliona utofauti mkubwa sana.
Ukweli ni kwamba hata wewe akija mgeni/wageni jambo la kwanza utakalo waza ni sehemu ya kuwalaza pazuri na kula vizuri pia.
Sehemu ya kulala ikiwa mbaya hata wewe mwenyew utapachukia tu.
Kuna dogo yeye kipaumbele chake ni simu anapolala Net imetoboka mashuka hayaeleweki hata Rangi Kwa kifupi ni mchafu sana na ukweli Huwa halali kwakwe mara Kwa mara.
Lakini kubadirisha simu Kali Hadi unajiuliza Hela za kununua simu Kali namna hii Huwa anatoa wapi?
Basi jitahidi sehemu ya kulala pawe na hewa safi na yakutosha pia