Haya ndiyo mapendekezo ya ccm kuhusu rasimu ya katiba mpya..!!

Haya ndiyo mapendekezo ya ccm kuhusu rasimu ya katiba mpya..!!

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,801



[h=2]Monday, July 22, 2013 | 12:55 AM[/h]

Mapendekezo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wanachama na viongozi wake.

1.gif

UTANGULIZI

1.1 Mnamo tarehe 03/06/2013 Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilitangaza rasimu ya kwanza ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

1.2 Rasimu hii ya Katiba itajadiliwa katika mfumo wa aina mbili wa mabaraza:

Mabaraza ya Katiba ya Wilaya, ambayo yameshaundwa na yatatoa maoni yake kupitia mikutano itakayoitishwa na Tume ya Marekebisho ya Katiba. Mabaraza haya yanasimamiwa na Tume yenyewe.

Mabaraza ya Asasi, Taasisi na makundi ya watu wenye malengo yanayofanana kama vile vyama vya siasa na jumuiya za kidini na kadhalika. Mabaraza haya yanasimamiwa na Asasi au Taasisi husika.

1.3 Chama Cha Mapinduzi kimeshajiunda kama Baraza la Katiba la kitaasisi na kutambuliwa rasmi na Tume kwa barua Kumb.na. AB 76/386/57 ya tarehe 24/052013

1.4 Kwa kuzingatia kwamba Chama Cha Mapinduzi ni Taasisi muhimu na yenye masilahi makubwa katika upatikanaji wa Katiba Mpya, Kamati Kuu ya Halmashauri ya Taifa iliyokutana mjini Dodoma Tarehe, 10/6/2013, pamoja na mambo mengine ilielekeza kwamba uandaliwe utaratibu utakaohusisha utoaji wa maoni utakaotumiwa na wanaCCM kutoa maoni yao.

1.5 Madhumuni ya ufafanuzi huu ni kujenga uelewa wa pamoja wa maudhui ya Rasimu ya Kwanza na hivyo kuwawezesha wanaCCM kushiriki kutoa maoni yao kikamilifu kutoka ngazi ya matawi hadi taifa.

UTARATIBU WA KUTOA MAONI

2.1 Kwa upande wa matawi maoni yatatolewa kupitia mikutano

Kwa wilaya, mikoa na taifa. Maoni yatatolewa kupita halmashauri kuu zao.


2.2 Ili kupata mfumo wa aina moja wa kuijadili Rasimu ya kwanza na kutoa maoni, wanachama wanaelekezwa kuzingatia vigezo vifuatavyo:

-->Kuitaja sura ya Rasimu ya Katiba inayohusika
-->Kutaja ibara ya Rasimu ya Katiba
-->Kutoa maelezo juu ya Ibara hiyo (kama kuna upungufu au maoni mengine yoyote);
-->Mapendekezo ya marekebisho
-->Sababu za mapendekezo ya marekebisho hayo.




Read more: HAYA NDIYO MAPENDEKEZO YA CCM KUHUSU RASIMU YA KATIBA MPYA..!! - GUMZO LA JIJI
 
Tume mbele ya tume! Baada ya kuona Jaji Warioba hakuwabeba sasa magamba wameamuka. Ninauhakika maoni ya wasionapesa yatapuuzwa.
 
Mkuu nngu007 unaheshimika kwa habari zako, sijui kama ulijiridhisha kuwa habari hiyo na link vina maana kwa msomaji.
Promo kwa njia iliyotumika na ulivyotumika si njema.
 
Watu mnaotaka kupata wasomaji kwenye vi-blog vyenu na kutengeneza pesa kwa njia ya mgongo wa JF lazima JF itafute mbadala ya kupambana nanyi either kwa kulipa PESA, BAN au vyote kwa pamoja.

Hii tabia ya Kinageria lazima iangaliwe na JF ili kuepuka kuwaongoza wana JF kwenye mtandao ambayo haipaswi kusomwa na familia.
 
Mkuu haya sio mapendekezo, labda tuambie kuwa ni utaratibu wa wanachama wa ccm kutoa maoni yao kwenye baraza lao la katiba!

Vyovyote iwavyo!

Watalia sana lakini Mzee Warioba ameamua kustaafu na heshima KUU kwa Watanzania kwakuwaletea Katiba ya Watanzania wote sio katiba ya Lumumba!

Mzee kakataa kutumika na kijani!
 
CCM wana waraka weney zaidi ya kurasa 17... huo ndio tunaoutaka...
 
tunataka maoni@yenu, jana wakili pale ubumgo alisema kuwa nyie hamtaki tunu za taifa ziwe kwenye katiba na serikali tatu hamzitaki, ndio waraka wenu mliowapa tume ya katiba, unasemaje kuhusu hilo
 
Back
Top Bottom