Haya ndiyo matukio yaliyonifanya niidharau michuano ya Kombe la Mapinduzi

Haya yote ni kwa sababu Yanga kutolewa.
Kamati ya waamuzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF), imesema kuwa Mwamuzi Nasri Salum hakustahili kuipa Simba kona iliyoifanya ipate bao la kusawazisha, katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi, wakati ikicheza na Singida Fountain Gate jana kwenye Uwanja wa Amaan.

Katika mchezo huo, Simba iliibuka na ushindi wa mikwaju ya penalti 3-2 baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 katika muda wa kawaida wa mchezo.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Waziri Shekha amesema uamuzi wa kuipa Simba kona katika dakika za nyongeza, haukuwa sahihi na kwa mwamuzi huyo alifanya makosa, japo kamati hiyo haiwezi kumpa adhabu.

"Nilikwambia kwamba tutachunguza na tumekutana leo, tumebaini kwamba kulikuwa na makosa ya mwamuzi. Haikupaswa kuwa kona. Hakuna sehemu ambayo mpira ulichezwa na mchezaji wa Singida na kipa akaudakia nje, hivyo haikuwa sahihi kuwa kona,” amesema na kuongeza;

“Ni makosa ya kibinadamu na ndio kosa pekee tumeliona baada ya kupitia ripoti na marudio ila sehemu zingine zote alikuwaa sahihi. Uzito wa kosa alilofanya hautoshi kumpa adhabu refa huyo ukizingatia amekuwa akichezesha vyema mechi nyingi.”

Soma zaidi kwenye tovuti ya Mwananchi
(Imeandikwa na Khatimu Naheka)
#mwananchiupdates
#tunaliwezeshataifa
 
Hata Ulaya pamoja na kuwa na VAR makosa kama hayo yapo
 
ndugu kama tukiongea football ni ipi tuseme sababu ya kushangaa kuona mchezaji akiwa jukwaani kisha baadae kushiriki mchezoni kama kuna sheria ipo against hiyo ni ipi ili tujifunze wote
Mkiambiwa Simba ni kiwanda Cha wajinga mkubali, hivi unawezaje kumchezesha mchezaji ambaye hayupo hata kwenye orodha ya wachezaji wa akiba?.
 
Kitu kilichonifanya nidharau mapinduzi cup ni kitendo cha timu ya mlandege kukodi waxhezaji wa ndondo ili wawasaidie fainali
Punguza ujuha... Simba haikuleta mchezaji kufanya majaribio... Au sio ndondo?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…