Haya ndo mashitaka matatu aliyosomewa Sheikh Ponda mahakamani leo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363


Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoa wa Morogoro kujibu mashitaka matatu yanayomkabili ambayo ni kutotii amri halali, kutoa maneno yenye nia ya kuharibu imani za dini na kushawishi kutenda kosa.

Sheikh Ponda amefikishwa mjini Morogoro na helkopta ya jeshi la polisi majira ya saa tano asubuhi chini ya ulinzi mkali ambapo askari waliimarisha ulinzi kwa muda wote huku kikosi cha kutuliza ghasia FFU wakiwa na silaha mabomu na mbwa ambapo hali hiyo imesababisha kusimama kwa baadhi ya shughuli zingine za kiofisi katika ofisi zilizopo jirani na mahakama ya hakimu mkazi wakati kesi hiyo ikiendelea ...




Akisoma shataka mbele ya hakimu mkazi Richard Kabate , wakili mkuu wa serikali kanda ya Morogoro Benard Kongola amedai kuwa shekh Ponda anadaiwa kutenda makosa hayo matatu Agosti 10 mwaka huu majira ya jioni katika viwanja vya shule ya msingi kiwanja cha ndege manispaa ya Morogoro.




Katika shitaka la kwanza la shekhe Ponda anadaiwa kutotii amri halali ambapo shitaka la pili anadaiwa kutoa maneno yenye nia ya kuharibu imani za dini kwa kutoa maneno kuwa serikali iliamua kupeleka jeshi Mtwara kushughulikia suala la vurugu iliyotokana na gesi kwa kuwaua na kuwatesa wananchi kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wa Mtwara ni Waislamu.




Shitaka la tatu linalomkabili shekh Ponda ni kushawishi na kutenda kosa ambapo anadaiwa kuwa alitoa maneno ya ushawishi kwa kuwataka waislaam wasikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za misikiti kwani zinaundwa na Bakwata ambao ni vibaraka wa CCM na serikali, na kama kamati hizo zitajitokeza aliwaamuru wafunge milango na madirisha ya misikiti kuwapiga.



Baada ya kusomewa mashitaka hayo shekh Ponda anayetetewa na mawakili wasomi Barthoromew Tarimo na Ignas Punge alikataa mashataka yote matatu na hivyo upande wa mashitaka kupinga dhamana kwa madai kuwa shekh Ponda anatumikia kifungo cha nje na kwamba hakutakiwa kufanya kosa, hata hivyo anakabiliwa na makosa mengine.

Upande wa mashitaka umedai kuwa upelelezi umekamilika na kesi hiyo itasomwa tena Agosti 28 mwaka huu ambapo mstakiwa amerudishwa rumande kwa helkopta jijini Dar es salaam.




 
Hiyo helicopter ilitua kihonda uwanja wa ndege, au jamhuri karibu na makao makuu ya polisi?
 
Tunampa pole kwanza angepona hapo ndo taratibu zingine zifuatwe, hivi kuna kifungu chochote cha kisheria kinachoruhusu mtu kusomewa mashtaka akiwa katika hali ya maumivu mazito kama haya? Huruma na haki za kibinadamu hapa zifuatwe sawia.
 
Tunampa pole kwanza angepona hapo ndo taratibu zingine zifuatwe, hivi kuna kifungu chochote cha kisheria kinachoruhusu mtu kusomewa mashtaka akiwa katika hali ya maumivu mazito kama haya? Huruma na haki za kibinadamu hapa zifuatwe sawia.

Kwa nini hayo maswali usimuulize Ustaadh Kikwete Na IGP Mwema? Nadhani wao watakuwa na majibu mazuri!!
 
Sasa garama zote za kumlete na kumrudisha rumande Dar za nini?kwa nin asiwekwe mahabusu hapohapo Moro
 
Mi nasema kwamba ni bora kubaki na fikra hai za watu waliokufa kuliko kubaki na fikra zilizokufa za watu walio hai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…