Haya ni mapenzi au kulogwa?

Haya ni mapenzi au kulogwa?

sinforosa

Member
Joined
Jul 28, 2011
Posts
32
Reaction score
19
Jamani mi nahisi nimelogwa kila ninapota kuachana na huyu jamaa najikutanimerudiana naye, mbali navituko anavyonifanyia ikiwemo kunicheat na nimeshamfumania na mwanamke ambaye ni X wake mara kadhaa na kwenye simu wakiwasiliana lkn sibanduki hadi police tumeshafikishana na kumlaza ndani siku 1,baada ya kuniomba radhi nikamsamehe mwezi baadaye tukarudiana je hiki ni nn? huwa nawaza sana na hisi akili yangu ataniudhi sana eitha kwa ulevi au maneno mm ndo naumia kwa kumuwaza yeye, sili, silali kila dakika anaclick kichwani. Naomba mnisaidie humu jamvini ni nn hiki?

Hujaamua huna kurogwa wala nini, mnafanana tabia ndio mana unamsamehe na unaelekea afya yako huithamini sana,dunia ya leo kila mmoja anamuogopa mwenzie wewe ushamuona mtu hamuendani tabia bado unaomba ushauri shosti jipeleleze!

Hujalogwa wala hakuna kitu kama hicho.
Kwa maoni yangu kutakuwa na mambo mawili hivi. Kwanza inawezekana huyo jamaa amekugusa mahali ambapo hukuwai kuguswa na yeyote. Kwa kifupi, anakupatia hasa! Pili, itakuwa ni ujinga tu, unawasiwasi ukimwacha unaweza kujutia. Labda kwa kukosa mwingine, au kutazamwa vbaya na jamii.
Ushauri wangu, chukua maamuzi magumu. Kama ulishamfumania ujue na maradhi yanakunyemelea if not yet! Tafakari, chukua hatua!

Ni vibaya sana kuwa mtumwa wa mapenzi, hivi inawezekanaje kumpenda mtu ambaye si muaminifu kwako na we mwenyewe unajua kabisa? Uko ni kukosa kujiamini kama unaweza kumpata mtu mwingine ambaye haswa anastahili hiyo nafasi. Kumbuka kuwa magonjwa ni mengi sana hivyo kutochukua tahadhari mapema unaweza kujuta hapo mbeleni. Tumezoea kusikia migogoro kama hii baada ya ndoa kwani kunawakati wanando wanakuwa hawakujuana tabia vizuri kabla, sasa wewe unajua kila kitu alafu unafurahia tena ikiwezekana unafagilia ndoa kabisa. Hakuna uchawi wala nini ni wewe mwenyewe tu unavyocheza na akili yako tu, pole sana.

Inaonesha unampenda sana kwa sababu kwa hizo tabia ulizozisema mimi ningeshasepa siku nyingi kwasabau sipendi pressure ya mapenzi, kwa sababu unampenda enedelea kumuombea labda atabadilika zaidi ya hapo subiri kuachwa wewe.

Jamani mi nahisi nimelogwa kila ninapota kuachana na huyu jamaa najikutanimerudiana naye, mbali navituko anavyonifanyia ikiwemo kunicheat na nimeshamfumania na mwanamke ambaye ni X wake mara kadhaa na kwenye simu wakiwasiliana lkn sibanduki hadi police tumeshafikishana na kumlaza ndani siku 1,baada ya kuniomba radhi nikamsamehe mwezi baadaye tukarudiana je hiki ni nn? huwa nawaza sana na hisi akili yangu ataniudhi sana eitha kwa ulevi au maneno mm ndo naumia kwa kumuwaza yeye, sili, silali kila dakika anaclick kichwani. Naomba mnisaidie humu jamvini ni nn hiki?

Mapenzi kitu cha ajabu saana... hakina adabu wala hakijali kua ushakua
mtu mzima na ya paswa utulie.... Wee hapo hujarogwa dear... ni mapenzi,
na woote ambao wamejaliwa na maanani kujisikia hivo mie personally husema
wana bahati for it is a great feeling....

However mpaka ume notice kua kakushika masikio.... huwezi maliza nae mda
sasa for utambuzi ni first step, the second utashangaa siku hio from nowhere
umeamua kua s/he is not worth it! and you have to move on...

Hakuna kulogwa wala maradhi hapo na wala sioni kinachokuwekesha kwake wakati anakufanyia vituko mpaka kutembea na ex wake wakati upo. Jiondokee tuu mapema kama mmeshindwa kurekebisha tofauti zenu.

sijaona tatizo ambalo unafikiri umelogwa hapo,...suala ni kwamba ww na jamaa yako mnapendana na ndio maana unamlaza ndani lakn bado anakubembelleza mrudiane,......pambana kumbadilisha tabia kwani hizo ni kasoro ndogo ndogo na kwa wanaume wengi tuko hivyo

Jamani mi nahisi nimelogwa kila ninapota kuachana na huyu jamaa najikutanimerudiana naye, mbali navituko anavyonifanyia ikiwemo kunicheat na nimeshamfumania na mwanamke ambaye ni X wake mara kadhaa na kwenye simu wakiwasiliana lkn sibanduki hadi police tumeshafikishana na kumlaza ndani siku 1,baada ya kuniomba radhi nikamsamehe mwezi baadaye tukarudiana je hiki ni nn? huwa nawaza sana na hisi akili yangu ataniudhi sana eitha kwa ulevi au maneno mm ndo naumia kwa kumuwaza yeye, sili, silali kila dakika anaclick kichwani. Naomba mnisaidie humu jamvini ni nn hiki?

"Mapenzi yana run dunia" ~ alikiba

sijaona tatizo ambalo unafikiri umelogwa hapo,...suala ni kwamba ww na jamaa yako mnapendana na ndio maana unamlaza ndani lakn bado anakubembelleza mrudiane,......pambana kumbadilisha tabia kwani hizo ni kasoro ndogo ndogo na kwa wanaume wengi tuko hivyo

Mkuu mchumba/mke wako ana shida sana. Kama anakufumania au unarudi ukiwa chicha mbaya na matusi juu na bado yuko na wewe ana moyo sana

Au amekupa lile linani sijui.....Hakuna uchawi hapo umejiloga mwenyewe huyo jamaa ameshajua kwamba wewe huambiwi kitu kwake,hivi umeshawahi kuona inavokuwa kwa mtoto anayependwa na wazazi nayeye akagundua hilo anavyo behave?

Nafikiri, unajiambia mwenyewe kuwa huwezi kuishi bila huyo jamaa, ukiweza tu kutoa hayo mawazo kwenye akili yako baasi utaweza ku move on mpaka utashangaa

hujarogwa,ila umejiroga mwenyewe,hujiamini kwa huyo mtu.penda unapopendwa,usipende usipopendwa

Nafikiri, unajiambia mwenyewe kuwa huwezi kuishi bila huyo jamaa, ukiweza tu kutoa hayo mawazo kwenye akili yako baasi utaweza ku move on mpaka utashangaa

Ni ukweli kabisa ndo maana nipo hapa kuomba msaada.

hata kama unampenda SANAAAAAAAAA .... tafakari TABIA zake .............je
1. anastahili kuwa MUME wako ...............ufunge nae pingu za maisha????
2. anastahili kuwa BABA WATOTO wako??? awe kiongozi wa familia yako?
3. Ana hadhi ya wewe kumjulisha kwa marafiki/ndugu/jamaa -(kwa tabia yake) bila wewe kuona aibu??

kama majibu ni SIVYO.............basi TABIA ikufanye UFUTE HISIA ZA UPENDO KWAKE .... MUNGU ATAKUPA ANAYEKUFAA.... HE IS SOMEWHERE....
give it time ......mtukutana tu siku moja

Mkuu mchumba/mke wako ana shida sana. Kama anakufumania au unarudi ukiwa chicha mbaya na matusi juu na bado yuko na wewe ana moyo sana

mkuu mimi sinaga lugha za matusi by nature_jamii inanijua na mpnz wangu anajua,...ila hapo kwenye blue ndio penyewe nakua chicha ile mbaya,..ingawa yeye hapendi na wala hatumii kileo,...nafikiri simtendei haki ila ndio hivyo tena _mimi na beer damu*2

Na inaelekea na kukufumania kashakufumania maana kwenye ulevi kila kitu ni possible

Wewe hujarogwa wala nn, tena chunga sana na hako katabia chakujifanya unamapenz zaid ya dunia! angalia ulipotoka na unapoelekea, utapata umpendae/akupendae na kukuheshimu!!

Back
Top Bottom