Haya ni ya kweli?

Haya ni ya kweli?

Ethan Cruz

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2021
Posts
231
Reaction score
331
a4b0d90a2d9b4895e9d41dcb52e9a9a1.jpg

Haya ni ya kweli?
1. Sio wanaume wote wanaopenda michepuko
2. Sio wanawake wote wana mwanaume zaidi ya mmoja
3. Kuna wanawake hawana Boyfriend kabisa
4. Kuna wanaume hawana muda kabisa na wanawake.
5. Kuna wanawake bado ni bikira hata kati ya umri wa miaka 18-30. Bikira zipo.
6. Kuna baadhi ya wanaume hawajawahi kulala na mwanamke ingawa wana miaka 20-30
7. Kuna baadhi ya watu wapo kwenye mahusiano bila ya kukutana kimwili. Wana date lakini hakuna sex, mpaka watakapooana.
8. Wanaume wote hawapo sawa. Sio wote wanaofikiri mwanamke ni chombo cha starehe. Wapo wanaoheshimu wanawake.
9. Wanawake wote hawapo sawa na sio wote huvutiwa na pesa katika mahusiano, wanachotaka ni heshima, upendo na uaminifu.
10. Kuna watu karne hii bado ni waaminifu, hawawezi kusaliti na kukusababishia maumivu ya kihisia.

Watu hutofautiana sana tabia kutokana na malezi na misimamo binafsi.
Je haya ni ya KWELI au UONGO. Niambie.

#THEHOOD
 
Kweli tupu mkuu.

Kuna na sababu zinazofanya hayo yasionekane kweli, na mojawapo ni wengi kuumizwa hivyo kuona woye sawa. Lakini pia tabia ya binadamu kupenda kutopitia shida peke yake. Atajifariji kwa namna yoyote hata kwa kuchafua wengine.

Ndio maana hata hapa jf nyuzi nyingi za mapenzi basi jinsia ke huwa inashambuliwa kwa kucheat na kuhirahisisha zaidi ilhali kuna watu wasio na tabia izo.
 
View attachment 1865783
Haya ni ya kweli?
1. Sio wanaume wote wanaopenda michepuko
2. Sio wanawake wote wana mwanaume zaidi ya mmoja
3. Kuna wanawake hawana Boyfriend kabisa
4. Kuna wanaume hawana muda kabisa na wanawake.
5. Kuna wanawake bado ni bikira hata kati ya umri wa miaka
Ndiyo japo kwa asilimia chache 5/100
 
Kweli tupu mkuu.

Kuna na sababu zinazofanya hayo yasionekane kweli, na mojawapo ni wengi kuumizwa hivyo kuona woye sawa. Lakini pia tabia ya binadamu kupenda kutopitia shida peke yake. Atajifariji kwa namna yoyote hata kwa kuchafua wengine.

Ndio maana hata hapa jf nyuzi nyingi za mapenzi basi jinsia ke huwa inashambuliwa kwa kucheat na kuhirahisisha zaidi ilhali kuna watu wasio na tabia izo.
#fact
 
Watu wa aina zote hizo wapo.

Mambo mabaya ya mahusiano huwa yanavuma sana kuliko mambo mazuri. Ndio maana uwepo wa watu wote uliowataja upo lakini hauvumi
 
mimi sijui kuhusu yote ila namba 6 ni kweli. mfano ni mimi.
 
Kweli
Kweli
Kweli
Yani yote fact. Kuna nyuzi nikizisomaga naona watu wanadiscourage wenzao sana kuhusu kuitunza nafsi.

Lakini yanawezekana. Nawatakia heri katika kuyaishi maisha haya tumuombe Mungu atusaidie jamani.

Ni maisha peace sana. Cheers to you mleta mada
 
Back
Top Bottom