Haya sasa ni Maradhi ya Rais Magufuli

Singeona tatizo kama wale wanaomkosoa nao wangeruhusiwa bila bugudha. kutaka sifa tu ni maradhi mabaya sana. ni dalili pia ya kutojiamini
Mbona wengi tunamkosoa kwenye mitandao???
 
M
Mwisho wake ukawaje mkuu?
Jibu mbona rahisi sana? wenyewe wanasema THE REST IS HISTORY. Mwisho wa Mobutu unajulikana, na matokeo ya sera hizo ndio tunachokiona huko DRC. Swali ni je, tungependa na sisi tufike huko? TAFAKARI, CHUKUA HATUA MAPEMA!!
 
Watasema umetumwa na mabeberu
 
Mbona wengi tunamkosoa kwenye mitandao???
Kwenye mitandao hapa kuna demokrasia, kuna wanaomkosoa na wanaomuunga mkono. basi aache na huko kwingine kuwe na ulinganifu. Vyama vya upinzani, ambavyo vipo kisheria na vipo kumkosoa kisheria, vifanye kazi zao kwa uhuru. Wafanye mikutano na maandamano kama ilivyokuwa enzi za JK. Aachie bunge live ili wabunge wa upinzani wanaporusha nondo zao zisikike nchi nzima. Aache magazeti yaandike kwa uhuru. aache TV zitoe kwa uhuru. TV na magazeti wameadhibiwa sana hapa kati. sasa hivi waoga balaa. huo UPENDO wa kulazimisha ni MARADHI
 
Kwani yamekatazwa????? Ila ninavyoona mimi nikwamba 'mkate uliowekwa siagi huwa chaguo la kwanza na ule usio na siagi ndiyo hufuata.
 
Ni kweli usemayo. lakini kumbuka pia kwamba Magufuli ni Citizen namba moja. akipiga chafya tu nchi inatikisika. tumempa madaraka makubwa sana kuhusu hatma ya nchi yetu. hatuna njia ila kumzungumzia sana tu. Pia kusema ni bora kuliko kukaa kimya.
 
Wanaompimga Rais Magufuli Ni mafisadi na wauza madawa ya kulevya na wenye vyeti feki

Sisi Watanzania tunampenda Magufuli,hao wachache wanajiangaisha tu
Kama wanaompenda ni wengi,kwa nini hamtendi haki kwenye chaguzi zinazofanyika?Mara kuwanyima fomu za kugombea,kukwepa wasirudishe fomu,wanatekwa,kupigwa na uchaguzi ukifanyika matokeo hayaaminiki.Upendo gani huo?
 
Kwani yamekatazwa????? Ila ninavyoona mimi nikwamba 'mkate uliowekwa siagi huwa chaguo la kwanza na ule usio na siagi ndiyo hufuata.
Yamekatazwa? Hujamsikia JPM akisema sasa tuacheni tufanye kazi. anaamini kwamba wapinzani wakimkosoa hataweza kufanya kazi yake! udhaifu ulioje huo?

Nakubaliana na wewe kuhusu mkate wenye siagi. ila sasa kwa nini kama tunaamini kwamba watanzania wanaujua mkate wenye siagi, kwa nini tunawazuia kuchagua kwa uhuru? haya mafigisu kwenye uchaguzi ya nini? jibu ni kwamba tunajua kwamba kama watanzania wataachwa wachague kwa uhuru, CCM HAIPATI KITU, kama alivyowahi kusema HUMPHREY POLEPOLE enzi zile akiwa na akili zake timamu, kabla ya kuvuta BANGI YA CCM
 
Raisi wangu usitengeneze kuchukiwa hata kama tutapata mkate na asali tunahitaji faraja
 
Wanaompimga Rais Magufuli Ni mafisadi na wauza madawa ya kulevya na wenye vyeti feki

Sisi Watanzania tunampenda Magufuli,hao wachache wanajiangaisha tu
Zuzu kweli wewe, Bashite ana vyeti fake je anampinga mungufuli? Nyie Inzi wa kijani akili zenu mnazijua wenyewe.
 
Nimeishia hapo uliposema local channels zinasifia juhudi za mwenyekiti. Well! Kama kusifia maendeleo yetu ni dhambi, basi jiunge na Fox news ukamsifie Trump
 
. Kutoka hapa... Mpaka hapa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…