Haya ya Simba niliyatarajia toka jana kupitia Ahmed Ally

Haya ya Simba niliyatarajia toka jana kupitia Ahmed Ally

Dialogist

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2014
Posts
1,167
Reaction score
1,872
Wakati wa pre-match press conference, na kwa wale wataalamu wa saikolojia mtakubaliana nami kwamba Msemaji wa Simba na semaji la CAF Bwana Ahmed Ally alionesha ishara zote za Leo timu yake kutokuingia uwanjani.

Hii ni baada ya kua na muonekano usio changamfu, na hata baada ya kuulizwa swali na waandishi mbona leo hajachangamka kama alivyozoeleka na wakati "kesho" wana derby, kwanini ahamasishi mashabiki wao kujitokeza kwa wingi uwanjani kuishangilia timu yao ipate ushindi, Bwana Ahmed aliishia kujibu kifupi tu Swaumu kali.

Hii inatafsiri kwamba Huyu Bwana alijua kabisa kuna kitu kinafanyika nyuma ya pazia cha kuleta sababu ya wao kutokushiriki mchezo husika. Kwamba wafanye tukio lolote wapate sababu za kukimbia. Kumbuka Yanga yupo katika ubora mkubwa na Simba anajitafuta. Na mbaya zaidi kipa wao wanayemtegemea hatocheza na ukizingatia wamefungwa na Yanga mara kadhaa mfululizo. So kuruhusu kufungwa tena ni sawa na kuivunja timu vipande vipande. Hivyo kuongea lolote la kuhamasisha ilikua ni kupoteza muda wakati tayari wana maamuzi ya kukimbia mchezo.

Nawasilisha!!
 
Leo ni siku ya wanawake, simba wapo bridi kwaiyo hawatoi mzigo
 
Back
Top Bottom