Abdul-Aziz Ally Carter
New Member
- May 24, 2024
- 2
- 24
SIASA;
(i) Mfumo wa upigaji kura wa elektroniki,
Kuwe na mfumo wa kupiga kura na kuzihesabu kwa njia ya kielektroniki badala ya kutegemea vituo na karatasi za kupigia kura, Wananchi wanaweza kupiga kura kwa njia ya simu zao za mkononi au kompyuta ili kuongeza ufanisi na ni vyema mfumo huu ukaunganishwa na mfumo wa NIDA ili wapiga kura wajiandikishe kwa kutumia namba au kitambulisho cha Taifa,
Mfumo huu utaleta urahisi, kuongeza ufanisi na ushiriki wa wananchi katika michakato ya uchaguzi, utawezesha wananchi kupiga kura wakiwa mahala popote bila ya kwenda kwenye vituo vya kupigia kura hasa kwa vijana, watu wenye ulemavu na wananchi wanaokaa mbali na vituo vya kupigia kura, utapunguza msongamano kwenye vituo vya kupigia kura ,kupunguza gharama za uchaguzi kama vile gharama za wasimamizi wa uchaguzi na uchapishaji wa karatasi za kupigia kura,utawezesha Watanzania waliopo njee ya nchi kupata haki yao ya msingi ya kupiga kura.
(ii) Ushirikishwaji wa wananchi kwa njia ya kura ya maoni na ombi la wananchi,
Wananchi wawe na uwezo wa Kushiriki moja kwa moja kwenye michakato wa maamuzi kuhusu masuala muhimu ya Taifa kwa njia mbili (2),
(a) Kura ya maoni,Ili kuwa na utawala wa kidemokrasia imara ni vyema kuwashirikisha wananchi kwenye michakato ya maamuzi, wananchi wapewe haki ya kupiga kura kwenye masuala mbalimbali kama vile mabadiliko ya Katiba, Sera za Umma na masuala mbalimbali yanayoigusa Jamii, kwa kufanya hivyo kutaongeza uwajibikaji wa serikali kwa wananchi.
(b) Ombi la wananchi, kuwe na ukarasa rasmi wa serikali uliopo kisheria kwa ajili ya wananchi kufungua na kusaini, njia hii itasaidia wananchi kuwasilisha maoni, mapendekezo na maombi yao kwa mamlaka kwa urahisi, itachangia kushinikiza serikali kufanya mabadiliko ya kisheria, kikanuni na kisera.
UCHUMI;
Maboresho ya sekta ya kilimo
(a) Kuanzisha mfumo wa kilimo cha umwagiliaji, ili kuwezesha shughuli za kilimo kuendelea hata wakati wa kiangazi na hivyo kupunguza athari za kupoteza mazao kwa sababu ya ukosefu wa maji, mfumo huu pia utasaidia kupunguza utegemezi wa mvua za msimu na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, pia itapelekea uwepo wa uhakika wa mazao kwa matumizi ya chakula na biashara na kuepusha mfumuko wa bei za vyakula hasa nyakati za ukame.
(b) Kuanzisha Bima ya mazao, Kuna umuhimu mkubwa wa kuanzisha Bima ya mazao ili kumlinda mkulima dhidi ya hasara zinazosababishwa na majanga ya asili kama vile ukame na mafuriko, magonjwa ya mazao au hatari nyingine zinazowakabili wakulima.
Msuko mpya wa sekta ya Madini;
(a)Iundwe sera inayotekelezeka ya uwazi wa sheria na mikataba ya madini,
Mikataba yote ya madini ichapishwe katika tovuti za wizara ya madini na maktaba za serikali, kuweka wazi taarifa za kifedha zinazohusiana na mikataba ikiwamo malipo ya serikali kama vile Kodi, Ushuru na tozo nyingine pamoja na gharama za uendeshaji ili kuleta uwazi, uwajibikaji na usawa katika sekta ya madini.
(b) Kuwe na mkataba wa makubaliano kati ya Kampuni za madini na wakazi wa eneo la migodi (wenyeji), mkataba ueleze fursa za ajira kwa wazawa na utunzaji wa mazingira, pia Kampuni za madini zinapaswa kulipa Ushuru au Tozo kwa serikali ya eneo husika na malipo yatumike kwenye maendeleo ya jamii kama vile Elimu, Afya na miundombinu,
Hii itawezesha pande zote mbili kunafaika na shughuli za uchimbaji madini na hii mikataba iwe kisheria na iwekwe wazi kwa Umma wa Watanzania.
Maboresho ya sekta ya Uvuvi;
Kuanzishwe mfumo wa mgawanyo wa kima cha uvuvi, Ili kuzuia uvuvi uliopitiliza hasa katika ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika na Bahari ya Hindi kwa wavuvi binafsi na Kampuni za uvuvi, kipimo kiwe katika mfumo wa kilogramu na tani, hii itasaidia uhifadhi wa rasilimali za uvuvi endelevu,kuzuia uvuvi kupita kiasi, kuhakikisha samaki wanaendelea kuzaliana na kustawi na kudhibiti uvuvi haramu.
JAMII;
(i)Maslahi ya wafanyakazi;
(a) Iundwe sheria ya kima cha chini cha mshahara inayotekelezeka, Ili kulinda Maslahi ya wafanyakazi katika sekta za Umma na sekta binafsi ni muhimu kuwa na sheria bora na inayotekelezeka ya kima cha chini cha mishahara na kuwe na maboresho ya sheria hii mara kwa mara ili kuendana na mabadiliko ya kiuchumi na kupanda kwa gharama za maisha na si kuacha kiwango cha mshahara kaumuliwa kwa makubaliano ya waajiri na waajiriwa au waajiri na taasisi za wafanyakazi, hii itasaidia kuboresha hali ya maisha ya wafanyakazi,
(b) Iundwe Bima ya fidia ya muda mfupi kwa wafanyakazi wote walifanya kazi kwa miezi 12 na zaidi kisha kuachishwa kazi kwa sababu zilizo njee ya uwezo wao kama vile kupunguzwa kwa idadi ya wafanyakazi au maendeleo ya teknolojia.
(ii)Maboresho ya mfumo ya Bima
Iundwe sera ya huduma ya Afya bila malipo,
Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) uchangiwe kupitia kodi za wananchi na Ruzuku kutoka serikalini ili kuwezesha kila Mtanzania kuwa na uwezo wa kupata huduma za Afya na kujikinga na hatari za kifedha zinazotokana na malipo ya gharama kubwa za matibabu, hii itasaidia kupunguza idadi ya vifo vya wananchi vinavyosababishwa na kushindwa kumudu huduma za matibabu, huduma hii ihusishe kumuona daktari, Dawa, vipimo na huduma za upasuaji.
(iii)Iundwe Tume ya Uadilifu wa polisi, Itakayokuwa na jukumu la kuchunguza tuhuma za ukiukwaji wa maadili ya maafisa wa polisi, kupitia Tume hii Raia wawe na uwezo wa kuripoti matukio ya unyanyasaji wa polisi, pia ipewe mamlaka ya kufanya uchunguzi huru.
(iv) Maboresho ya Mfumo wa Magereza;
(a) Mfumo wa magereza utoke kuwa wa adhabu na kuwa wa kurekebisha, kuwe na programu za mafunzo ya ufundi na usaidizi wa kisaikolojia.
(b) Iundwe sera ya kuwalipa wafungwa kwa kazi za uzalishaji wanazofanya ndani na njee ya magereza.
(c) Kwa kushirikiana na Taasisi za kibenki, Iundwe akaunti ya wafungwa kwa lengo la kuwawekea akiba kutoka kwenye kiasi cha pesa wanacholipwa kwa kufanya shughuli za uzalishaji.
(v) Ili kukabiliana na aina mbalimbali za majanga ya asili kama vile vimbunga, Mafuriko, Moto wa misitu, Maporomoko ya ardhi, Milipuko ya Volkano na Tsunami, liundwe shirika la kitaifa la usimamizi wa majanga. Shirika litengeneze mfumo imara wa kukabiliana na majanga, sera za kupunguza athari zitokanazo na majanga, uwezo wa kuhimili na kurejesha hali ya kawaida baada ya majanga pamoja na mfumo wa tafadhari.
Sheria
Maboresho ya mifumo ya kisheria ya TAKUKURU,
(a) Mfumo wa uteuzi wa TAKUKURU urekebishwe badala ya Mkurugenzi mkuu na naibu mkurugenzi mkuu kuteuliwa na Rais, Iundwe kamati huru ya uteuzi inayotokana na wafanyakazi wa taasisi zisizo za kiserikali na mashirika ya kitaaluma.
(b) Kwa mujibu wa sheria ya Rushwa ya 2007, Ibara ya 6 ibara ndogo 1 Rais ndiye muangalizi mkuu wa TAKUKURU, Jukumu hili liondolewe na kuhamishiwa kwenye kamati za Bunge.
Imeandaliwa na,
Abdul-Aziz A. Carter
Mwanafunzi - UDSM
carterally002@gmail.com
0742935585

Upvote
1