SoC04 Haya yafanyike ili kuifikia Tanzania tuitakayo

SoC04 Haya yafanyike ili kuifikia Tanzania tuitakayo

Tanzania Tuitakayo competition threads

DUASMaka

Member
Joined
May 27, 2024
Posts
5
Reaction score
2
Tanzania ni nchi yenye rasilimali nyingi kiasi cha kuweza kuihudumia dunia katika mambo mbalimbali kama chakula, sekta ya madini na hata mavazi endapo zitatumika vema. Tangu kipindi cha uongozi wa Rais na Baba wa taifa J.K Nyerere maneno haya yamekuwa yakisemwa na viongozi na wanamapinduzi mbalimbali na hata kufanya wanafunzi kufundishwa hivyo.

Tanzania yenye nguvu ya kesho inategemea uwezo wa watu wake katika kutumia rasilimali ambazo kila anayepita kama kiongozi anakiri kuwa ni utajiri mkubwa tulionao katika nchi yetu.

Lakini imekuwa kama vigumu fulani hivi kuzifanya rasilimali hizo kuwa utajiri halisia kwa nchi na watu wake. Je unafikiri ni nani ana wajibu wa kuzifanya rasilimali hizo kuwa mali?

Makampuni mbalimbali ya nchi za nje huona fursa na kuja kuwekeza Tanzania na kuwafanya watu wa nchi hii kuwa nguvu kazi na siyo wanufaika nambari moja kwani watu hawa hufurahia mishahara tu baada ya malipo ya kazi hizo na kutotaka kujua nini kinaendelea baada ya uzalishaji huo. Lakini basi hili sio suala la msingi kulizingatia kama mwananchi wa chini kwani yote hayo hufanyika chini ya mamlaka husika za serikali yetu ya Tanzania.

Kupitia serikali hii mjadala huu wa "stories of change" umepewa nguvu hata kuruhusu wananchi kuchangia mawazo yetu ili kupata Tanzania bora ya kesho chini ya dira inayoandaliwa ya miaka ya 2025-2050.

Taifa lifanyaje kuzifikia ndoto za kuitoa Tanzania ilipo na kwenda mahali pazuri zaidi ya tulipo?

Ni vema kujua kwamba dunia ya sasa inahitaji watu wenye ubunifu mkubwa sana kisayansi, teknolojia na ustadi mbalimbali wenye kujenga uchumi shindani ambao utakuwa nguzo kubwa katika uwekezaji mbalimbali, kwa ufupi nguvu ya kiuchumi ndiyo yenye nafasi kubwa katika dunia ya sasa.

Sote tunatambua kuwa kwa miaka tisa mpaka sasa [2015-2024] masomo ya sayansi yamepewa kipaumbele mashuleni ili kupata wasomi wengi wa sayansi hata kuifanya elimu kuwa bure ili kila mtanzania afikie ndoto zake kimasomo. Jambo hili limepelekea wanafunzi wengi kuweza kufikia elimu ya juu ya chuo kikuu yaani degree na kuendelea.

Mpaka sasa Tanzania inao vijana wengi mtaani ambao ni wasomi, weledi na wenye uwezo wa kukufanya mabadiliko katika nchi yetu endapo serikali itawatumia katika mlengo uliopangwa ili kuijenga nchi yao.

Vijana wengi waliohitimu elimu ya vyuo vikuu wamekosa ajila za serikalini na kuamua kujiajili kwa nafasi zao ndogondogo. Hivyo basi tunapata majibu kwamba vijana ambao serikali imeasomesha kwa elimu bure hadi vyuo vikuu wamekuwa wajasiliamali wadogowadogo na maana yake ni kwamba nchi imewapa elimu kubwa vijana wake lakini wanaitumia kidogo sana ukilinganisha na matarajio ambacho sio sawa na viwango tunavyohitaji ili kujenga nchi yetu kufikia ndoto zake.

Tutawezaje kuifanya nguvukazi hii inayotumika kwa uchache au vibaya kutupatia pato kubwa na maendeleo katika nchi yetu? JESHI ni chombo cha wazalendo, waadilifu na wachapakazi wenye kuleta ushawishi katika kujenga nchi kwenye sekta mbalimbali.

Tunaweza kujenga nchi yetu kwa kuunda chombo chenye kujitegemea cha kizalendo, kiadilifu na kichapakazi kwenye nchi yake kwa kutumia vijana wasomi na wenye maarifa makubwa yaliyotolewa bure na serikali yetu tukufu chini ya Raisi Dkt Mama Samia Suluhu Hassan.

Jeshi hilo liwe ni ajira kamili kwa vijana wanaomaliza vyuo tu na kiwe ni kitengo maaluumu cha uzalishaji mali chini ya jeshi kama ilivyo sumaJkt.

Majukumu ya jeshi hili liwe ni kilimo, ufugaji na uvumbuzi wa kisayansi ambalo litaifanya Tanzania kuwa na mashamba makubwa na mengi yatakayouza mazao yake nchi zote duniani na kukifanya kuwa chombo muhimu cha kukuza uchumi wa nchi na watendaji wake kulipwa kama wafanyakazi wa umma.

Uwepo wa jeshi hili itakuwa ni ajira kwa vijana na matumizi mazuri ya rasilimali watu katika nchi yetu utakaofanya nchi kuweza kufikia lile dhumuni la kuwa nchi yenye utajiri usio hewa na kuwa faida kwa nchi na wananchi wake.

Lakini pia wazo hili linaweza kutufanya kuwa na wananchi wenye amani ya kiuchumi na kuondoa uhalifu mdogomdogo katika mitaa yetu unaochangiwa na ukosefu wa ajira.

Kwa kumalizia , Tanzania sio mahali pa watu wake kukosa ajira, tunahitaji mtazamo mpya wenye uthubutu kama huu uliooneshwa na Rais wetu Dkt Mama SS Hassan kwa kuifanya nchi yetu kupanga mlengo wa miaka 25 mbele ili kuibadilisha nchi yetu katika nyanja za kiuchumi, siasa na maisha bora kwa watu wake.

Chapisho hili ni wazo kutoka kwa DUASMaka, haruhusiwi mtu yeyote kuchapisha au kutumia bila idhini.
 
Upvote 2
Mpaka sasa Tanzania inao vijana wengi mtaani ambao ni wasomi, weledi na wenye uwezo wa kukufanya mabadiliko katika nchi yetu endapo serikali itawatumia katika mlengo uliopangwa ili kuijenga nchi yao.
Tinao mtaji wa rasilimali watu wenye elimu sasa.

Jeshi hilo liwe ni ajira kamili kwa vijana wanaomaliza vyuo tu na kiwe ni kitengo maaluumu cha uzalishaji mali chini ya jeshi kama ilivyo sumaJkt.
Saaaaaafi, kuunganisha watu kama jeshi kuifikia adhima moja ni muhimu sana. Juhudi zilizoelekezwa vema zina matokeo.

Chapisho hili ni wazo kutoka kwa DUASMaka, haruhusiwi mtu yeyote kuchapisha au kutumia bila idhini.
Hahahahaaaaaaaah! Haiya chief
 
Back
Top Bottom