SoC04 Haya yafanyike katika kukuza sekta ya elimu kwa miaka ijayo

SoC04 Haya yafanyike katika kukuza sekta ya elimu kwa miaka ijayo

Tanzania Tuitakayo competition threads

Conqueror771

New Member
Joined
Jul 31, 2023
Posts
3
Reaction score
1
Kwanza nipende kushukuru kwa kupata kufahamu juu ya fursa hii, watanzania wote wanaweza kutoa mawazo yao tofauti tofauti,

Pia nichukue nafasi hii kuipongeza serikali toka awamu ya tano na ya sita walipojitahidi kufanya vema katika sekta ya elimu kwa kumruhusu elimu iwe bure pasipo kulipa ada kutoka shule za msingi mpaka kidato cha sita,
Pia serikali imefanikiwa kuongeza idadi ya wanufaika wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu pamoja na kuwaongeza fedha kwa ajili ya kujikimu wakiwa vyuoni (meals and accommodation) kutoka 520000 mpka 600000

KATIKA KUKUZA SEKTA YA ELIMU KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI NINGESHAURI SERIKALI IFANYE YAFUATAYO

. Mpaka sasa tunaona kuna shule chache za vipaji maalumu ilihali watu wenye uhitaji wa shule hizo wakiwa ni wengi
Hivyo kwa miaka ijayo serikali ingejitahidi kujenga na kutenga angalau shule angalau 3 kwa shule za msingi na shule 3 kwa shule za sekondari ambapo zitakuwa ni shule za wanafunzi wenye mahitaji maalumu

. Pia ningeshauri serikali kubadilisha mtaala wa elimu kwa shule za sekondari,(kidato cha kwanza hadi cha sita) na kuruhusu kuwepo na somo la kujifunza lugha za alama na kama atafaulu vizuri atapangiwa katika combination yake kwa kidato cha tano na sita na baadae kwenda chuo kikuu tofauti na sasa ambapo somo hilo mwanafunzi anakutana nalo akiwa chuo kikuu na kuliona gumu
kwa kufanya hivyo serikali itasaidia kupata kupata walimu wengi na watu professional wa lugha za alama ambao watasaidi katika shule za vipaji maalumu na sekta zingine


YAFUATAYO NINGESHAURI SERIKALI ILI WANAFUNZI WAENDELEE KUNUFAIKA ZAIDI NA MIKOPO HII

1) Kwanza ningeshauri mikopo wanayopatiwa vyuoni mfano kwa sasa ndani ya semester moja mwanachuo anapewa pesa ya kujikimu mara mbili kwa semester, wengi wao huwa wanachezea maana mtu anakua amepata pesa kubwa kwa mara moja means atumie 600000 kwa miezi miwili hivyo inapelekea mtu kutumia pesa vibaya na kuimaliza ndani ya muda mchache

USHAURI ningeshauri serikali ibadili mfumo wa ugawaji ambapo mwanafunzi atatakiwa kupewa shilingi 300000 kila mwezi ili kupunguza matumizi mabaya
Kuliko sasa hivi wanavopewa 600000 kwa mara moja na itamlazimu akae nayo ndani miezi miwili

2) kwa kua mikopo kwa wanafunzi ilianzishwa ili kusaidia wanafunzi wasiokuwa na uwezo wa kugharamia gharama za masomo vyuoni
Ningeshauri kwa miaka ijayo wabadili sheria ambapo kwa wazazi ambao wamefanikiwa na watoto wao wamebahatika kupata mikopo hiyo wazazi pia washiriki katika kurudisha mikopo hiyo... kwa kutumia namba za nida na mifumo mingine serikali itaweza kuwakata asilimia kadhaa wazazi ambao wameajiriwa na watoto wao wamepata mikopo ya elimu ya juu na pesa hizo zikaendelea kutumika katika kuongeza mikopo kuliko kusubiri mwanafunzi aajiriwe ndipo aanze kukatwa kwenye mshahara wake

3) Pia kuliko kusubiri mwanafunzi huyo apate ajira ndio aanze kurudisha pesa za mkopo alizopewa na serikali ningeshauri serikali ibadili mifumo ya urudishwaji wa pesa hizo Kwa kuweka mifumo thabiti ambayo hata ikiwa mtu huyo ataanzisha biashara binafsi basi serikali iwe inakata asilimia kadhaa kutokana na kipato chake,

Mwisho ningeshauri kutokuogopa kuchukua maamuzi magumu ambayo kwa muda huo yataumiza lakini yanakuwa na matokeo chanya kwa maisha ya baadae pia tusiangalie nikifanya jambo fulani nitaonekanaje mbele za watu, au watu watanichukuliaje, cha muhimu ni kuzingatia malengo

AHSANTENI NAOMBA KUWASILISHA
 
Upvote 2
USHAURI ningeshauri serikali ibadili mfumo wa ugawaji ambapo mwanafunzi atatakiwa kupewa shilingi 300000 kila mwezi ili kupunguza matumizi mabaya
Kuliko sasa hivi wanavopewa 600000 kwa mara moja na itamlazimu akae nayo ndani miezi miwili
Heeeh, sasa mwanachuo mtu mzima kabisa aendelee kubaniwabaniwa hivyo.

Ni lini atajifunza kuwajibika kwa 'funds' zinazopita mikononi mwake? Tunatengeneza Taifa la namna gani kwa hali hii?


kwa wazazi ambao wamefanikiwa na watoto wao wamebahatika kupata mikopo hiyo wazazi pia washiriki katika kurudisha mikopo hiyo... kwa kutumia namba za nida na mifumo mingine serikali itaweza kuwakata asilimia kadhaa wazazi ambao wameajiriwa na
Again. Kuwawajibisha wazazi kwa masuala ya watoto wao wenye umri zaidi ya miaka 18!!. Hapana tafuta njia nyingine ya kumuwajibisha mkopaji mwenyewe. Na njia iliyo bora zaidi ni ;
A. Kumuajiri kisha ukate mshahara.
B. Kuweka mazingira rasmi ya kujiajiri na ukate faida na kodi juu.
 
Habaniwi ila ni mipango tuu ni saw na wew sasa hv mzazi awe anakupa pesa ya matumizi ya mwaka kwa mara moja au kwa awamu tofauti???

Pia kusema funds zinazopita kwake means atakua ametolea jasho itamuuma kuchezea
Hakuna inaemuumua kuchezea boom
 
Umekosea mkuu, wazazi kukatwa is not fair, mpaka watoto wamepewa mkopo it means wazazi wameshafanyiwa assessment na kuona hawawezi kuwalipia watoto wao..

..nimeipenda hii ya kulimit kiwango cha pesa kwa wanafunzi wasipewe hela kubwa yote, hata UK maintenance loan inatolewa kwa installment...nimekupa vote...
 
Umekosea mkuu, wazazi kukatwa is not fair, mpaka watoto wamepewa mkopo it means wazazi wameshafanyiwa assessment na kuona hawawezi kuwalipia watoto wao..

..nimeipenda hii ya kulimit kiwango cha pesa kwa wanafunzi wasipewe hela kubwa yote, hata UK maintenance loan inatolewa kwa installment...nimekupa vote...
Una uhakika wote wanaopata huo mkopo wazazi hawajiwezi??? Hata mm nipo chuo bado nawaona na waliokosa pia wapo ambao wazazi hawajiwezi
 
Back
Top Bottom