Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Hakika wanachadema mpo kwenye wakati mgumu kuliko wakati mwingine wowote ambao mmepitia kama Chama
Kuna viongozi wengi na wanachama wenu wengi wameondoka kutokana na sababu moja au nyingine lkn naweza sema halikuwashtusha kama ambavyo litawashtusha hili ambalo litatokea sasa hivi
Ni wazi kabisa Mwenyekiti wenu wa sasa mh Mbowe ni kipenzi chenu kikubwa na mh Tundu Lisu Makamu Mwenyekiti nae ni kipenzi chenu pia,this time vipenzi vyenu vimeamua kama noma na iwe noma
Naamini kabisa kwa namna yoyote ile itakayo fanyika kumuondoa Lissu katika mchakato wa kugombea Uenyekiti ima iwe halali au kibabe utaleta athari kubwa sana katika chama chenu,na ndio hapo tutashuhudia taulo likitupwa ulingoni
Siamini hali hiyo ikitokea kama mh Lissu atabakia kuwa mwanachama hai wa Chadema,maana akibakia itakuwa unafiki tu ila moyoni mwake atakuwa hana mori na moyo wa kubakia hapo
Inafahamika kwamba Lissu amejizolea umaarufu mkubwa sana kwa ujasiri wake na upambanaji wake wa kudai haki na usawa hapa nchini kwetu,binafsi ingawa ni mwanachama au mshabiki wa Ccm lakini namkubali huyo mwamba sana
Endapo ataondoka Chadema kwa figisu ya aina yoyote ile basi mjue Chadema mtakuwa mmerusha taulo ulingoni katika siasa za vyama vingi na huenda mkawa kama vingine ambavyo vilisharusha taulo ulingoni kitambo tu kama Nccr Mageuzi na vinginevyo
Kwa namna hutuba ya Lissu nilivyo isikia hakika inaonyesha kabisa kuna haja ya kufanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi ndani ya Chadema,hapo inahitaji hekima na ukomavu wa kisiasa wa mh Mbowe asema inatosha sasa na kumpa kijiti mh Lissu
Ukiweka uchawa pembeni kwa kila mwanachama wa Chadema mwenye akili huru na uelewa wa kutosha ataona kabisa anayefaa sasa kuwa kamanda mkuu ni mh Lissu
Mungu ibariki Afrika na Mungu ibariki Tanzania
Asanteni kwa kunisikiliza
Ni hayo tu!