Haya yalimkuta Ronaldinho miaka mitano iliopita...

Gang Chomba

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2008
Posts
20,649
Reaction score
4,786
Miaka mitano iliopita kiungo mshereheshaji wa zamani wa baadhi ya vilabu vya Soka barani Ulaya ikiwemo AC Milan Ronaldo de Assis Moreirra maarufu kama Ronaldinho Dinho Gaucho alipata ajali baada ya Gari lake pendwa kuacha njia na kuingia mtaroni.

Ilianza kuwa siku nzuri sana kwa huyu bwana lakini baadae iligeuka kuwa siku mbaya iliomtoa machozi.

Dinho Magic ambae duru mbalimbali za Soka ziliwahi kukiri kuwa hakika yeye ndie Mtume na Nabii wa mwisho wa mchezo huo ambae kiungo wa zamani wa Real Madrid na Chelsea Claudio Makelele alipata kukiri kuwa mara zote alipomuangalia Gaucho akiwa na Uwanjani basi alijiona yeye hajui Mpira, alipata ajali siku ambayo Mama yake Mzazi alikuwa akiadhimisha siku ya kuzaliwa.

Bi Dona Miguelina Elói Assis dos Santos wenyewe hupendelea kumuita (Miguelina Elói Assis dos Santos) ambae ni Mke halali wa Mzee Joao de Assis Moreirra alikuwa akisherekea siku yake ya kuzaliwa, na kwa hamu na gamu alikuwa akimsubiri mwanawe kipenzi Dinho Gaucho kwani mwanawe huyo alikuwa kamuahidi Mama Yake zawadi nzuuri ya Birthday.

Huku akiwa anawahi tukio la Birthday lililokuwa linafanyika katika Mji ambao Gaucho alizaliwa mji wa Porto Alegre ghafla tukio la ajali likatokea na kisha Gari hilo likaingia mtaroni.

Hakukuwa na majeruhi yeyote na hata yeye Gaucho alitoka akiwa mzima lakini mwenye majonzi makubwa huku akibubujikwa na machozi.
Gaucho aliwaza mbaali ya kuwa atakosa kumpatia kwa wakati zawadi aliomuahidi Mama yake, kitu ambacho kilimuumiza sana.

Huku akiwa kama kachanganyikiwa sambamba na kutiririkwa na machozi, alitokea kijana mmoja ambae alihamaki baada ya kumuona Nyota wa Mchezo wa Soka ambae anamuhusudu saana.

Kijana huyo hakutaka kujivunga bali alionesha mahaba yake ya wazi kwa Gaucho bila kujali kuwa Gaucho yupo katika wakati mgumu hapo.

Kijana huyo alipenya baadhi ya vizingiti na hatimae akafika alipo mbarikiwa huyo na kumsalimia kwa furaha ile hali Gaucho akiwa analia.
Baada ya hapo Kijana huyo alimueleza Gaucho kuwa anaomba apige nae picha (selfie) ya pamoja kwani hajui kama ataweza tena kupata nafasi hio maishani, na kwamba amekuwa akiiota nafasi hio kwa kipindi kirefu sana.

Kipenzi cha Watu Dinho Gaucho, alikubali ombi la kijana huyo na kupiga nae picha ambayo ilikuja kutoa taswira mbili tofauti.
1. Ilionesha Sura ya majonzi
2. Ilionesha sura ya furaha.

Je unajuwa baada ya hapo nini kilitokea kwa Kijana huyo?!

Endelea kunywa Mtori...Nyama utazikuta chini.

 
Guardiola anakabidhiwa tu Barcelona anafanya mkutano na waandishi wa habari anasema "Mimi na benchi la ufundi tunataka kuibadilisha hii timu kimbinu lakini Ronaldinho, Deco na Eto'o hawapo katika mipango yetu"

Kipindi cha Rijkaard hao 3 walikua ni miungu, huwagusi, so watachelewa mazoezini wataharibu dressing room lakini hawaguswi. Guardiola akawashangaza watu kwa kuwataja miungu kwamba hana mpango nao.

Mchezaji mmoja alisema "Ronaldinho alikua bora lakini mpira ni mazoezi, unaweza usiwe unafanya mazoezi lakini mwishowe ni itaonyesha tu kwamba wewe ni mvivu"

Kwa maoni yangu alistaafu akiwa bado ana umri wa kucheza ila huo uvivu ndiyo lilikua tatizo haswa.
 
Huyu zidane na de lima ndo walishushwa na MUNGU Kucheza mpira duniani.Hawa wengne kina messi na wenzake wamejifunzia hapa hapa duniani
 
Chomba unatuzingua mufti, kwa hiyo tusubiri part 2, kuwa serious kidogo.
 
Lakini si ndio huyu huyu aliyekuwa anawahi mazoezini na kuchelewa kuondoka km cr7 afanyavyo!!??
Na katika ubora wake gaucho mwili wake ulikuwa unaonekana fiti kweli kimazoezi, nakumbuka game ya barca vs arsena hleb sijuk na flamini yule, walienda kuhangaika na mwili wa gaucho mpaka nikacheka.. Kina gattuso walipata tabu nae mnoo, mvivu wa mazoezi ingekiwa ngumu kufanya yale kwa dk90.

Gaucho mambo ya nje ya uwanja yalimzidia.
 
Mkuu hapo mawazo yangu ni hayo ya kusema naamini umri wake ulikua unadai.

Mawili ya juu siyo yangu.
 
Mkuu vizingiti vipo wapi mbona inaonekana ni road za uswazi kabisa hapo.

Tunasubiri muendelezo
 

Ronaldinho made Barca, Barca made Messi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…