Abeid Abubakar
Takwimu nyingi zinaonyesha kuwa Watanzania wengi wanajihusisha kwa namna moja au nyingine na kilimo.
Kwa mfano, utafiti wa nguvu kazi ya taifa wa mwaka 2014 ambao bado unatumika kama rejea nchini, unataja bayana kuwa asilimia 66.3 ya Watanzania wameajiriwa au kujiajri katika sekta ya kilimo.
Ni dhahiri kuwa sekta hii ina umuhimu wa kipekee na ndio maana imekuwa ikinasibishwa na uti wa mgongo wa Taifa letu.
Hata hivyo, ninapotazama mwenendo wa sekta hii, napata shaka kama nchi hatujawa makini na kilimo, ndio maana mpaka leo zaidi ya nusu karne tangu tupate uhuru, bado tunategemea kuagiza mafuta ya kula, sukari, maziwa na bidhaa kadhaa ambazo malighafi zinatokana na kilimo.
Makala haya yanajaribu kuangazia baadhi ya mikakati ambayo pengine inaweza kuokoa kilimo chetu hasa tukilenga kundi kubwa la vijana.
Mikopo
Kwa muda sasa Serikali kupitia halmashauri imekuwa ikitoa mikopo ya kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. Utaratibu unazitaka halmashauri kutoa asilimia 10 ya mapato yake kwa makundi hayo. Lakini mikopo hiyo licha ya kusuasua, bado haijawa na tija sana kwa upande wa kusaidia makundi haya hasa vijana kujikita kwenye kilimo kama sekta ambayo naamini inaweza kuwatoa kimaisha.
Ni wakati sasa kukawa na utaratibu maalumu kuwa eneo mojawapo la watu kuwekeza wanapopata mikopo hiyo iwe ni kwenye kilimo. Ikiwezekana hili liwe sharti kuu.
Hata hivyo, makala haya mbali ya mikopo, inashauri utoaji wa ruzuku (grant) badala ya mikopo. Hivi karibuni niliuwa nasoma taarifa ya Mfuko wa Pembejeo wa Taifa ukitoa wito wa maombi ya mikopo ya pembejeo za kilimo, mifugo na uvuvi.
Katika tangazo hilo kulikuwa na maelezo kuwa muda wa mkopo ni miaka miwili na riba ni 8% kwa mtu binafsi na 6% kwa vikundi.
Pamoja na nia njema, nikiri kuwa hilo la riba tayari linaweza kuwa kikwazo kwa walio wengi. Riba ndogo au kubwa bado ni janga na wengi wanakwama hapo.
Inawezekana kwa kuwa lengo ni kuimarsia sekta hii yeti, pembejeo hizi zingetolewa kwa njia ya ruzuku ili wengi zaidi wanufaike, huku kukiwa na masharti na vigezo makini sambamba na usimamizi wa matumizi ya fedha hizo.
Kutoa ruzuku hakumaanishi ni kutoa fedha za bure, bado wanaopewa watalazimika kusimamiwa na wale watakaotapanya fedha hizo wachukuliwe hatua kazi za kisheria.
Halmashauzri zitenge maeneo
Nashauri kuwe na mkakati wa kila halmashauri, tarafa, kata au hata vijiji kutenga ardhi maalumu kwa ajili ya vijana kujikita kwenye shughuli za kilimo zitakazosimamiwa kikamilifu na wataalamu wa Serikali.
Hilo likifanyika sambamba na kutoa hamasa kwa vijana kujikita kwenye shughuli hizo, vijana wapewe elimu ya kilimo cha kisasa na cha kibiashara, elimu ya ujasiriamali, mahesabu, masoko na mnyororo mzima wa thamani kwenye kilimo ili hata kama wengine hawatolima, wajikite katika shughuli zinazohusiana na sekta hiyo.
Uhamaishaji huu wa vijana kwenye kilimo nashauri ujumuishe kilimo cha vizimba (block farming) Hapa vikundi vya vijana vinakatiwa idadi maalumu ya ekari za kulima ambazo watazimudu chini ya usimamizi.
Wazo jingine linaloweza kusaidia kuinua kilimo chetu, ni kutumia mfumo wa skimu za umwagiliaji kwa lengo la kuepukana na kilimo cha kutegenea mvua.
Ikiwa leo tuna skimu za umwagiliaji kwa kilimo cha mpunga, tunaweza pia kuchuka utaratibu wa kuwa na skimu za umwagiliaji kwa mazao ya kimkakati kama mahindi kwa ajili ya nafaka, alizeti, karanga, ufuta kwa ajili ya utengenezaji wa mafuta ya kula au mazao jamii ya mikunde au hata kilimo cha matunda na mbogamboga.
Kama imewezekana katika mpunga kwa kuwa na skimu maeneo mbalimbali ya nchi, mfumo huo unaweza pia kutumika kwa mazao mengine.
Kwa mfano, moja ya sababu kuu ya uhaba wa mafuta ya kula uloikumba nchi miezi iliyopita, ni uzalishaji mdogo wa alizeti hasa mikoa inayostawisha zao hilo kama Singida kwa sababu ya mvua kuwa chache, hivyo viwanda kukosa malighafi. Lakini kama alizeti mkoani Singida ingekuwa inalimwa kwa mfumo wa skimu za umwagiliaji, kilio cha ukosefu wa malighafi kisingesikika.
Kilimo shuleni
Kama tujuavyo, shule hasa za msingi na sekondari, ndio maeneo ya kufinyanga watoto. Namna tunavyowalea shuleni ndivyo watakavyokuja kuwa wakiwa ukubwani.
Kilimo hakina budi kuhimizwa tangu shuleni kama iliyokuwa zamani wakato wa sera ya elimu ya kujitegemea.
Turudishe kilimo shuleni kuanzia ngazi ya msingi na kwa shule za vijijini kuwe na utaratobu maalum wa kila shule kuwa na mashamba darasa. Kupitia mashamba hayo sio tu wanafunzi watapata maarifa ya kilimo lakini mavuno yatakuwa sehemu ya kipato cha shule na hata kutumika kama chakula hasa kipindi hiki tunachosisitiza utoaji wa lishe kwa wanafunzi.
Hili halina budi kwenda sambamba na uanzishwaji wa shule maalumu za kilimo kwa ngazi ya sekondari kama ilivyokuwa kwa shule kama Ruvu, Kibiti na Dakawa zilizojengwa kwa msaada wa serikali ya Cuba ili kuwa chachu ya kuandaa wataalamu wa kilimo.
Shule hizi enzi hizo zilisheheni vifaa vya kisasa kama matrekta na hivyo kutoa fursa kwa wanafunzi kupata maarifa ya kilimo kwa vitendo.
Kanda za kilimo
Hivi sasa ni kama kilimo kinafanywa hobelahobela, hatulimi kimkakati kwa kutazama umuhimu wa kanda zetu kimikoa na jiografia yetu. Nashauri mazao kulimwa kikanda, kwa mfano tuwe na kanda maalumu zilizojikita kwenye kilimo cha nafaka, kanda nyingine zijikite katika matunda, ufugaji wa nyuki, mbogamboga na kadhalika. Hii itasaidia hata katika usimamizi wa kiserikali kwa kupeleka nguvu zinazohitajika mahala fulani na kwa malengo maalumu ya kimkakati.
Hata hivyo, hili likifanyika haimaanishi maeneo mengine wasilime la hasha! ila msukumo na jicho la Serikali viwe katika uzalishaji wa mazao katika kanda husika ambazo zitakuwa zikilima kwa kiwango kikubwa.
Dhana ya kilimo-burudani
Naweza nisiwe nimepatia sana kimsamiati, lakini hoja hapa ninayopendekeza ni kukifanya kilimo kuwa burudani hasa kwa kuwa walengwa tunaotaka wajikite huko ni vijana ambao aghalabu hutekwa na burudani.
Kama ilivyo kwa dhana ya elimu- burudani (edutainment), hilo pia linaweza kufanyika kwa vijana. Wasomi wa kilimo wabuni mifumo itakayochanganya shughuli za kilimo na burudani hususan michezo inayowavutia vijana.Hii itasaidia hata kuondokana na ile dhana kuwa kilimo ni matatizo na adhabu.
Abeid Abubakar ni mkazi wa Dar es Salaam. Anapatikana kwa barua pepe: abeidothman@gmail.com

| Skimu za umwagiliaji mazao mbalimbali |

Upvote
1