Hayati Dkt. Magufuli ndio mkombozi wangu

Hayati Dkt. Magufuli ndio mkombozi wangu

Abuu Said

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2015
Posts
4,010
Reaction score
4,763
Habari wana Jamii Forum great thinkers wenza ngumu

Leo naomba nikiri kwamba aliyekua Rais wa awamu ya 5 Dr. John Pombe Magufuli ndie mkombozi wangu ktk mahangaiko ya Kimaisha. Nimeiona watu wengi humu JF na kule Twitter wakimdhihaki mpendwa wetu yule km vile hakuna mema aliyoyafanya.

Ngoja nianze sasa ni jinsi gani JPM alivyonisaidia. Nimemaliza elimu yangu ya Diploma in Mechanical engineering pale DIT mwaka 2014 baada ya hapo nikawa nahangaika kutafuta ajira bila mafanikio nikaanza kufanya kazi za kujitolea ktk Gereji na Ofisi mbalimbali kwa ajili ya kusukuma maisha kabla sijapata ajira rasmi.

Ukaingia uchaguzi wa 2015 ambapo JPM alifanikiwa kuchukua Urais hali kidogo ilikua ngumu kule kwenye kujitolea ikabidi niache kazi kutokana na Pesa kua ngumu, kulikuwa na ule msemo wa JPM umeenea kwamba watu warudi vijijini wakalime pesa itakua ngumu na kweli pesa ilikua ngumu kila unapokwenda kuomba kazi wanakwambia hawa waliokuwepo tunataka kuwapunguza.

Basi ktk kuchanganua akili nikaona bora na mimi nirudi mkoani ambapo kwetu ni Tanga kwenye wilaya moja ndogo kiuchumi.
Nikarudi zangu kuanza mikakati ya kimaisha na kweli nilifuata sera ya JPM ya kutumia rasilimali ya Ardhi nikaanza kulima lakini wakati naendelea na harakati zangu Wilayani kwetu tukapata ugeni wa PM Kassim Majaliwa ambapo ktk hutuba yake aliongelea kuhusu mkopo kwa vijana inayotolewa na Halmashauri.

Katika hutuba ile nikaondoka na hilo nikakusanya vijana wenzangu na kuwashawishi jambo la kuunga kikundi na kwenda kuomba mkopo Halmashauri.

Mwanzo tulikua na wazo la kuomba mkopo kwa ajili ya kilimo lakini wakati tunafuatilia kusajili kikundi tulikutana na Afisa vijana wa wilaya yetu akatushauri tuombe mkopo kwa ajili ya kufungua kiwanda cha Tofali ukizingatua kutokana na JPM kuja na sera ya nchi ya viwanda basi tukakubali lile wazo tukaomba mkopo asilimia 4 ya vijana kwa ajili ya kununua Mashine za kisasa za ufyatuaji tofali na Halmashauri ilikubali ombi letu na kutupatia mkopo huo na mimi ndio Mwenyekiti wa Kikundi.

Na sasa nimefanikiwa kujiajiri na kuachana na kutafuta ajira km vijana wengi akili zao zilipokua.

Kwahiyo JPM ameniweka kwenye mwanga kutokana na sera zake na kututaka vijana tujishughulishe.

Naambatanisha na Picha tuliopiga wanakikundi tulipokuja kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru.

Wasalaam

IMG-20210626-WA0029.jpg
 
Yaani ukikimbizwa na Nyoka ukaangukia kwenye shimo, huko ukaokota 700000 iliyofichwa na mwizi unamshukuru Nyoka kama Mkombozi wako au yule Mwizi aliyeficha hela? Hebu tueleze uhusiano wa moja kwa moja wa hiyo JPM kuwa mkombozi wako?
1. Kuweka nidhamu kwa Watendaji ikafikia hatua Watendaji wa Serikali kuwa waoga na kufanya kile wanashoamrishwa.

2. Sera yake ya Viwanda ilifanya Halmashauri kutoa kiasi kikubwa cha fedha.

3. Kubana fedha ikanifanya nihame mjini na kuja kutafuta changamoto nyingine kijijini.

Yapo mengi ila hizi zinatosha
 
Wewe utakuwa na tabia za kiroho mbaya, muuaji, mtekaji na maskini wa akili na roho.

Matendo ya magu ukiwa ndiye role model wake basi wewe ni mchawi
 
1. Kuweka nidhamu kwa Watendaji ikafikia hatua Watendaji wa Serikali kuwa waoga na kufanya kile wanaxhoamrishwa.
2. Sera yake ya Viwanda ilifanya Halmashauri kutoa kiasi kikubwa cha fedha....
Acha kulalamika. Bunge la ccm waliopita bila kupingwa na baraza lote la mawaziri wote wamepitishwa na huyo huyo magufuli. Ni vile tu hayupo lakini haya ndio alikuwa anaelekea kufanya na yametimia. Lipa kodi acha malalamiko
 
Nchi hii vijana hawatakiwi ni lzm wakomolewe,vijana wamejiajiri kwenye mitandao wanakutana na panga,kesho bodaboda nao zamu yao
 
Back
Top Bottom