Hayati Magufuli alijaza makada wa CCM kwenye teuzi za Serikali, hawa ndio wapiga dili wenyewe, Rais Samia asiwachekee

Kila siku tunasoma vitabu vya ujasusi wa kiuchumi ili tusonge kama taifa lakini unakuta umweka kada asiye na maono unatagemea afanye maendeleo gani kwa taifa, sema Kama taifa tumeshawatenga wasomi wenye elimu, ujuzi na weledi tunaangukia kwa wanasiasa mambumbumbu yasiyo na dira, mama anza kupunguza makada wasio na tija kwa taifa
 
Unakuta DG wa TTCL anavaa mashati ya chama ofisini!
 
Nasikia hadi kwenye vyombo vya ulinzi na USALAMA makada wwalingizwa bila kufata vigezo
Hili nimelishudia kwa macho yangu. Nilikutana na baadhi ya makada waliotoka umoja wa vijana wameajiriwa na chombo nyeti cha Ulinzi. Yaani ni weupe kichwani sikuamini macho na masikio yangu, baada ya kushuhudia utendaji wao uliokuwa wa kiwango cha chini kabisa.
 
Nia yake ilikuwa mbaya kwa Taifa hili kuteua watu wanaofikiria matumbo yao na kuwapendelea watetezi wake na wewe ukiwa miongoni mwao,kama Mama Samia atakuwa ameligundua hili,basi hamna shaka kuwa na wewe mtoa post unastahili kuwajibishwa kama Ole Sabaya.
 
January sio kada?
Makala sio kada?
 
Mataga wote wakijirudi kama wewe itapendeza sana. Sifia panapostahili. Na kosoa penye kasoro. Sio kusifia kila kitu.
 
Hahahaaaa....... Bwashee mimi ni mstaafu!
 
Kumbe ufisadi wa kutisha ulianzia awamu ya tano ya Bwana Chato😁😁😁
Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…