Hayati Magufuli alikataa kukosolewa akiwa hai, sasa watu wanamkosoa akiwa amekufa

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
11,550
Reaction score
40,697
Vita kali ya maneno ya kumkosoa na kumdhihaki Magufuli inayoendelea sasa huenda ni matokeo ya kitendo cha Magufuli kukataa kabisa yeye na utawala wake kukosolewa akiwa hai.

Hichi kinachoendelea ni matunda ya tabia ya Magufuli mwenyewe ya kupenda kusifiwa tu huku akiwadhihaki watangulizi wake. Japokuwa haipendezi lakini huo ndio ukweli mchungu.

Kila zama na kitabu chake, kuimba ni kupokezana.
 
tena umenikumbusha …Nyerere mwenyewe na mengi mazuri yasiyomithilika aliyoyafanya kwa Taifa hili alipokuwa anatuaga Diamond Jubilee hakuwa anajikweza sijui kusema nikiondoka nani atayafanya haya na yale na badala yake akaomba radhi kwa pale alipokosea na kwa uungwana kabisa akawaomba radhi Wasaidizi wake wakuu kina Kawawa kuwa kuna nyakati walikosolewa na kukashifiwa kwa kusimamia yale waliyokuwa wametumwa na yeye
Yule jamaa kweli alikuwa mshamba sana. Hata Nyerere aliyetuletea uhuru alifikia hatua ya kutaka viongozi/watu wajikosowe wenyewe, achilia mbali kukosolewa. Sasa yeye eti asifiwe tu. Na watu wa TBC wakatimiza hilo 100%.
 
Vita kali ya maneno ya kumkosoa na kumdhihaki Magufuli inayoendelea sasa huenda ni matokeo ya kitendo cha Magufuli kukataa kabisa yeye na utawala wake kukosolewa akiwa hai.

Hichi kinachoendelea ni matunda ya tabia ya Magufuli mwenyewe ya kupenda kusifiwa tu huku akiwadhihaki watangulizi wake. Japokuwa haipendezi lakini huo ndio ukweli mchungu.

Kila zama na kitabu chake, kuimba ni kupokezana.
Na wajifunze kwa hili walen wote waliomsifu na hata kufikia kumfananisha na Mungu.
Bado nao wote moto utawawakia chini ya ardhi hii

Sent from my SM-A115AZ using JamiiForums mobile app
 
tena umenikumbusha …Nyerere mwenyewe na mengi mazuri yasiyomithilika aliyoyafanya kwa Taifa hili alipokuwa anatuaga Diamond Jubilee hakuwa anajikweza sijui kusema nikiondoka nani atayafanya haya na yale na badala yake akaomba radhi kwa pale alipokosea na kwa uungwana kabisa akawaomba radhi Wasaidizi wake wakuu kina Kawawa kuwa kuna nyakati walikosolewa na kukashifiwa kwa kusimamia yale waliyokuwa wametumwa na yeye
Huo ndio ungwana sio yule fascist Jiwe aliekuwa anataka yeye asifiwe na kushangaliwa kama ndio mwenye kugawa pumzi kwa Watanzania,ikafikia stage anatufanyia maigizo barabarani anamopita ili mradi tuu sifa apewe yeye tuu.
 
Back
Top Bottom