Hayati Magufuli alitufundisha walalahoi kuchagua walalahoi wenzetu

Hayati Magufuli alitufundisha walalahoi kuchagua walalahoi wenzetu

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Kuna watu hawawazi kama kuna watu kupata milo miwili kwa siku ni shida.

Unakuta baba ni fundi na anategemea akitoka akapata kibarua ndiyo nyumbani wanasonga ugali, baba ni machinga akitoka akatembeza vitu mitaani ndiyo familia inakula.

Wapo watu tangu wamezaliwa hawajawahi kukosa chai kuanzia kwa wazazi wake mpaka kwake yeye mwenyewe.

Binafsi nilimwelewa sana JPM alivyokuwa akiwatetea hawa watu wa chini kuwa wasinyanyaswe.

Rai yangu walalahoi tumtafute mtu aliyewahi kupitia maisha haya ya huku chini atatufaa sana kwa kuwa mwelewa katika kusimamia haki zetu.
 
Hakuna nchi inaendeshwa na mlala hoi. Hayati Magufuli hakuwa mlala hoi.
Nilichokisema ni mtu ambaye amewahi kupitia maisha ya ulala hoi anakuwa anaelewa wanachokipitia walalahoi.

Kama ulivyokuwa mtoto uliwahi kushindia uji tu bila mlo, umewahi kufukuzwa kwa kukosa karo huwezi kumsumbua mtu anayeishi maisha hayo
 
Kwahiyo unahisi Meko alikuwa mlala hoi 😂 watanzania walirogwa na nani sijui!

Waziri Miaka 20 !
Kasoma Masters Uingereza
Rais miaka 6 alafu anajichotea pesa!
Ana ma hotel na miradi kibao


Unasema ni MLALA HOI DAH

NI BORA JF IVAMIWE NA FACEBOOK KULIKO BADOO NA INSTAGRAM 😂
 
SmartSelect_20210928-182522_Kamusi Kuu ya Kiswahili.jpg
 
Ni hero kwa watu wenye uelewa mdogo. Lakini kiuhalisia alikuwa dhalimu aliyejificha kwenye uhuru wa biashara holela. Hakuna hero jizi la kura.
ataendeNilea kuwa hero kwa watanzania wengi sana. Mungu aendelee kumlaza mahala pema.
 
Uliza wamachinga au wachimbaji wadogo wa madini watakupa jibu zuri

Kuruhusu biashara holela haikuwa utatuzi halisi la matatizo ya wamachinga. Wachimbaji wadogo kuna lipi la ajabu?
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Vyovyote vile sisi tunamkubali sana hakuna maneno yatayotubadilisha
Ukitaka kuujua ujinga wako ulipofikia
Tizama Majibu Yako. Unalazimisha Sisi Ingali Ni Wewe Pekee .Jisemehe wewe Acha kulazimisha .Sema Mimi Na Sio Sisi
 
Back
Top Bottom