Hayati Magufuli amewafanya Watanzania wawe mafukara zaidi

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Hi!
Sekta ya ajira
Serikali yake ilishindwa kuajiri angalau kwa wastani wa kupunguza jobless kwa kila familia na ukoo.
Sasa hakuna Rais ataweza kufix suala la unemployment Tanzania. Mpaka sasa wapo madaktari wanajitolea na kulipwa kidogo ili tu siku ziende. Hali hii haijawahi kutokea tangu tupate uhuru. Sekta binafsi ambaye ndiye mwajiri mkubwa mnajua kilichotokea. Wengi walipoteza kazi.

Kilimo
Sekta ya kilimo aliipiga vibaya mno. Hata wizara yenyewe ya kilimo ilikuwa haipewi pesa za maana.

Uvuvi
Huko nako hakuacha , wavuvi wakubwa walinyooshwa mpaka walinyooka.

Biashara
Aahhh huko ndo usiseme neno. TRA walikuwa wanatembea na mapolisi wenye SMG kila wakati. Maduka maelfu kwa maelfu yalifungwa. Mimi ni mmoja wa waliofunga maduka yao.

Watumishi wa Umma
Tulinyooshwa haswa kwa kisingizio kuwa anafanya maendeleo. Itachukua miaka mingi kidogo Watanzania kusogea mbele.

Binafsi sio maskini wala si fukara, nina ajira permanent, nina miradi ya hapa na pale kiasi kwamba naweza kuishi out of employment, ila Watanzania wengi ni mafukara. John Pombe kachangia sana hili
 
Kipindi cha JK vyuo na shule za secondary viliongezeka kwa kasi kubwa, kwanini hujafanya analysis ya matokeo ya shule na vyuo hivyo

Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app
 
Sawa wewe utakuwa kwenye nchi yako wakati sisi tunapewa
Sikia mkuu swala la ajira ni duniani kote nu social problem
Kuhusu biashara na ukusanyaji wa kodi niswala la TRA wanaokadilia kodi sizan kma wanakadilia kubwa kiasi iko ila pia wanafanya kazi kwa maagizo kutoka serikali kuu

Embu niambie kwa mfano vitu hivi vichache katiba mpya italekebisha nini?
 
We kweli huna akili umaskini wako ni wewe mwenyewe kuutoa au kuukumbatia.
 
Chuma JPM endelea kupumzika kwa amani, ni miaka miwili tangu ututoke lakini Mafisadi, wezi wa mali ya umma na watumishi wavivu wameshindwa kuendelea na maisha yao bado wapo kwenye taharuki ya utendaji kazi wako, hawaamini kwamba uliwafumbua macho watanzania na kuwaonyesha ya kuwa tukiamua, tunaweza. Pumzika kwa amani Mwamba
 
Katiba mpya itaweka mifumo huru na imara ambayo haiingiliwi na wanasiasa, wakwepa kodi wakubwa wa nchi hii ni wana siasa ambao hupiga simu moja tu mzigo inapita, niambie leo hii unaweza kuzuia mzigo wa Mwigulu Nchemba? yule ni mfanyabiashara mkubwa ana petrol station kibao na mabasi.
 
Haya ukiipata katiba mpya usisahau kuniambia
 
Umerudi na genge lako kututoa Relini.

Hapendwi mtuu hapa mpaka kieleweke, rudisheni rushwa mliokula hiyo.

Tuanataka Bandari yetu!
No to DPW no to Neo-Colonialism
 
alisema mtamkumbuka, na mtamkumbuka kweli ngoja sukari ifike Sh. 5000/-kg
 
Kabla hujalaumu angalia uwiano wa vyuo vinavyotapika Graduates na ofisi. Kumbuka mtu anaajiriwa mara moja na kukaa kwa miaka mingi ofisini. Kama ofisi ina staff 20 ndani ya mwaka na wanao graduate ni candidates 50,000 unawagawanyaje. Hata serikali iajiri vipi hao watu ni wengi mno. Una retain wafanyakazi 20 for 5 years nje kuna watu laki 2 wenye sifa. How do you cope with that situation. Asilaumiwe mtu hata wangeajiri toka 2015 still graduates wengi wangekosa kazi tu.
 
Kama wewe ulivyo fukara kichwani
 
Ninawachukia ccm mpaka naumwa

Hamnaga ubongo nyinyi! Nyinyi ni aheri shetani awachukue tu tulishawachoka

Unaandika upumbavu tu hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…