Hayati Prof.Kighoma Ali Malima, Kiongozi na mzalendo wa kweli Tanzania

Hayati Prof.Kighoma Ali Malima, Kiongozi na mzalendo wa kweli Tanzania

hassan kisabya

Senior Member
Joined
Jun 14, 2014
Posts
165
Reaction score
109
Hayati Prof.Kighoma Ali Malima, mzaliwa Pwani, wilaya ya Mkuranga Tarafa ya Mkamba, mwasisi wa NRA, ni miongoni mwa viongozi wenye sifa ya uadilifu waliopata kutokea Tanzania, Ni mwanamapindizu wa fikra hapa Tanzania, aliwahi kuutahadharisha umma kuwa "Kama yupo mtanzania anayeunda chama ili kupambana na chama kingine,basi mtu huyo amepoteza uzalendo na dira, aliamini uundwaji wa vyama utambue kuwa vyama vinakuja sio kupambana na chama kingine bali watu waunde vyama ili kupambana na shida na kero za watanzania"
Fikra hizi Ndio zinaifanya NRA Kuwa taasisi pekee tanzania iliyo mstari wa mbele kuuonea huruma umma na kuweka mbele maslahi ya taifa ,viongozi wa sasa wakiongozwa na mhe Rashid Mtuta (M/kiti Taifa),tumeendelea kuenzi fikra hizi
 

Attachments

  • IMAG0512_1_1_1.jpg
    IMAG0512_1_1_1.jpg
    199.4 KB · Views: 420
  • P+8.jpg
    P+8.jpg
    98.8 KB · Views: 306
Subiri subiri kidogo mkuu, wananzengo watakuja tu kuchangia, mi napita tu.
 
Nasikia alikwiba mijifedha ya hazina akiziweka London siku alipokwenda kuzichukua akakuta Kikwete kazichukua presha ikampanda kifo kikamchukua.
 
Oya karibu rweganzala upate supu ya sato,wananzengo tumejaa hapa.
 
Huyo mtu alikuwa na udini wa hali ya juu, aliachia ngazi kwa shinikizo toka bungeni, alikuwa anatoa misamaha ya kodi hadi taifa lilikuwa linaambulia 10% tu ya kodi zote. Kighoma Malima hakuwa mtu, alikuwa ni balaa, kusitaafu kwwake Ni Rais Mwinyi alimfuata akamwambia Shehe sasa hubebeki achia ngazi utunze heshima.
 
Back
Top Bottom