Hayawi hayawi, hua. (Kozi ya Upwork ipo jikoni)

Joined
Apr 5, 2024
Posts
81
Reaction score
117
1718641257690.png

Habari wanaJF,

Ni mimi tena, na natumaini kuwa upo vizuri unaposoma maneno haya. Leo imekuwa siku ya Idd kwa ndugu zangu waislamu, na wasabato fulani wapo kwenye msimu wa makambi. Yote mema....

Ee bwana, juzi kati nilizungumzia kozi yangu ya Upwork nitakayoitafsiri kwa ajili ya kusaidia wabongo kuweza kupata kazi mtandaoni. Uzi wenyewe huu hapa: Changamkia fursa za kazi mtandaoni. Lakini kuna haja ya hili kwanza...

Nilipata some feedback (mrejesho), na nimeamua kuwa ntaendelea kwa watakaokuwa tayari kwa safari hii.

Leo nimeanza rasmi kazi hii na itaendelea kwa wiki kadhaa. Ntakuwa nashusha dondoo za hapa na pale, na mbinu muhimu za kuzingatiia endapo utataka kufanikiwa.

Katika utangulizi tutazingatia vitu muhimu vya kuzingatia endapo unataka kufanikiwa Upwork (hasa unapoanza):

Account and Profile Integrity (Jinsi ya Kulinda hadhi ya akaunti yako)
  • Kamwe usidanganye kuhusu utokako (km, usijiandikishe kuwa unatoka marekani wakati upo hapo Sinza kwa wajanja), fani/utendaji (utashindwa kufanya kazi usizoweza), uzoefu au kazi ulizofanya. Sifa ya kwanza ya kufanikiwa ipo katika kuwa mkweli.

  • Usiunde akaunti zaidi ya moja. Upwork inaruhusu akaunti moja tu kwa kila mtu. Akaunti nyingi inaweza kufanya mfumo ukushuku na kukutema.

  • Tumia lugha na picha sahihi. Usitumie lugha au picha ambayo inaibua maswali.
Communication and Client Interactions (Jinsi ya Kuwasiliana na Wateja Wako)
  • Usifanye kazi nje ya Upwork. Kufanya hivyo ni kukiuka masharti ya mfumo, na unaweza ukapoteza akaunti yako.

  • Usimpe yeyote taarifa binafsi kabla ya mkataba wa kazi. Baadaye tutaongelea mikataba ya kazi. Hakikisha kuwa mawasiliano yote yakafanyika ndani ya mfumo wa Upwork, na sio vinginevyo, hadi mteja atakaporidhia kufanya kazi na wewe.

  • Ishi ndani ya uhalisia. Ofa yoyote ikiahidi mbingu duniani, chukua tahadhari. Usije ukalia kwa kupigwa na kitu kizito kichwani. Endapo kuna jamaa anajaribu kukutafuta na uelewi anacholeta, toa ripoti upwork kuhusu hili, kwa usalama wako na wa wengine.
Pointi za Ziada
  • Baadaye, tutakuja kuongelea jinsi ya kutafuta kazi (proposals and bidding), na mkataba na malipo (payments and contracts)
  • Chukua muda kusoma mkataba wa Upwork vizuri ili kuepuka makosa ambayo yatakucosti baadaye.
  • Jenga uzoefu na portfolio kwa ajili ya kupata wateja wengi.

Aisee subiri niachie hapo kwa leo. Kama wewe ni mzoefu, hebu ongezea hapo kwa nilichokiandika. Aidha, ungependa tuzungumzie nini katika uzi zijazo? Naomba kusikia kwako pia.
 
View attachment 3019557

Sawa
 
Back
Top Bottom