DR Mambo Jambo
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 11,622
- 26,005
SOLIDARITY!
Mei Mosi, au Siku ya Wafanyakazi Duniani, ilianza kama harakati ya kutetea haki za wafanyakazi katika karne ya 19.
Mnamo mwaka 1886, maandamano ya wafanyakazi nchini Marekani yalifanyika kudai saa za kazi zisizozidi masaa 8 kwa siku. Tukio hili linajulikana kama "Haymarket affair" ambapo polisi walifyatua risasi dhidi ya waandamanaji, na kusababisha vifo vya waandamanaji na polisi pia.
ambapo siku ya nne ya maandamano mtu asiyejulikana aliwarushia askari bomu na polisi walifyatua risasi na kupelekea vifo vya wafanyakazi na Askari pia
Baada ya tukio hilo, Mei Mosi husherehekewa kama Siku ya Wafanyakazi Duniani ambapo wafanyakazi hupata fursa ya kuwasilisha changamoto zao kwa waajiri.
Kutokana na tukio hilo, Chama cha Wafanyakazi cha Kimataifa (International Workers' Association) kilipendekeza kuitisha mgomo wa kitaifa tarehe 1 Mei, 1886, kudai saa za kazi zisizozidi 8 kwa siku.
Hii iliongoza kwa maandamano na migomo katika miji mingi duniani kote. Tangu wakati huo, tarehe 1 Mei imekuwa ikisherehekewa kama Siku ya Wafanyakazi Duniani, kwa kuenzi mapambano na mchango wa wafanyakazi katika kuleta mabadiliko ya kijamii na kiuchumi.
Solidarity Forever!