Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Wakati Mhe. Rais anaingia Madarakani aliwataka watendaji wa serikali kufanya tathimini kuhusu aina ya mifumo inayohitajika serikalini na kuboresha ufanisi.
Juzi Kati Tanesco walipata matatizo kwenye mfumo wa LUKU nakupelekea kukosekana kwa huduma hii.
Niliwaza sana kuhusu udukuzi wa kimtandao unaofanyika Duniani kwa sasa, nikajiuliza hatukudukuliwa? Je, malipo yetu ya mtandao yapo salama?
Hi nadhani ndiyo iliyonipelekea niwaze hatupigwi? Na Kama tunapigwa tunapigwa kiasi gani? Nani mwenye uhakika kwamba control number zinazotolewa mara mbili mbili siyo tobo la maafisa tehama na wakandarasi kuibia serikali? Nchi nyingi Duniani zinapigwa mabilioni kupitia mifumo, najiuliza sisi hapa kwetu usalama tumeutoa wapi wa mifumo yetu?
Je, watendaji wa serikali mtandao wanaelewa upo umuhimu wakupitia mifumo ya taasisi zote na benki kujiridhisha kuhusu malipo?
Enzi zetu wahasibu walikuwa wanatengeneza vitabu vyao vya risiti, je watengenezaji wa mfumo hawawwezi kujitengenezea control number au wadukuzi awawezi kuchepusha malipo kwenda kwenye akaunti?
Hebu serikali mtandao fanyeni tathimini bila kuwashirikisha Wataalamu wa ICT wa taasisi mbalimbali ambao naamini wanaficha ukweli wa mifumo kuonyesha inafanya vyema, watafuteni watu randomly na tengenezeni ukaguzi maalumu mtuakikishie fedha zetu zipo salama.
Maana yapo magazeti na vyombo vya habari vinaripoti wizi wa huduma zinazolipiwa kwa control number, huo wizi unafanyika kwa njia gani au wanajiandikia bila kujua huduma zinatolewa vipi?
Hazina mitandao si ya kulala ni kukekesha mnachunguza mianya na kuoziba