Hazina niliyorithishwa na mwalimu wangu Mzee Kissinger

Hazina niliyorithishwa na mwalimu wangu Mzee Kissinger

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
HAZINA NILIYORITHISHWA NA MWALIMU WANGU MZEE KISSINGER

Wanafunzi wote duniani hurithishwa hazina ya ilm katika vitabu na mfano wa hivyo kutoka kwa walimu wao baada ya walimu wao kuondoka duniani.

Mimi mwalimu wangu Mzee Kissinger kanirithisha maktaba yake mwenyewe yu hai pengine akichelea mmoja wetu asije kutangulia na ile hazina ikaanguka katika mikono siyo.

Mwalimu wangu akanirithisha hazina ya Maktaba yake wakati sisi sote tu hai tena miaka mingi iliyopita.

Naandika maneno haya huko machozi yananinyemelea machoni pangu.

Siwezi kumlipa mwalimu wangu kwa hisani hii kwani gharama yake ni kubwa mno huwezi kuipima ukaiwekea thamani.

Nitaweka machache kutoka Maktaba yangu hii ambayo waandishi wa Wasifu wa Julius Nyerere wameisifia kwa kusema ni kati ya maktaba bora walizoona katika utafiti wao wa historia ya maisha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
20200623_013102.jpg
20200623_012345.jpg
20200623_012435.jpg
 
Mzee Mohamed, Umemuaanda kijana ama mtu wa kurithi hazina hii? Na hizi historia adhimu unazotupatia kuna kizazi kitaendelea kurithisha kwa kizazi hadi kizazi?
 
Wee mtu ni nouma aiseee... ushauri wngu kwako..embu muandae mtu wa kuichunga hiyo maktaba..maana huo ni urithi wa nchi yetu hapo mbeleni
 
Wee mtu ni nouma aiseee... ushauri wngu kwako..embu muandae mtu wa kuichunga hiyo maktaba..maana huo ni urithi wa nchi yetu hapo mbeleni
Kanta...
Ondoa hofu In Shaa Allah vitu vyote vitakuwa salama kuweza kutumiwa na wengine.
 
Back
Top Bottom