Nilikuwa kwenye pita pita yangu mtandaoni kuhusiana na mikopo, nikakutana na Hazina Saccos Tanzania.
Miongoni mwa vitu vilivyonivutia ni pamoja na riba ndogo walizoziweka. Lakini nikajiuliza maswali yafuatayo:
1. Je huwa wanatoa mikopo kwa wakati? Yaani inachukuwa muda gani tangu kuomba mkopo mpaka kupewa? (Kwenye uhalisia)
2. Je unaweza kujitoa ikiwa bado unaendelea na utumishi wa umma ukataka kuacha uanachama? Kwa mfano kama ume-lose interest ya kuwa mwanachama na hauna deni?
Ninaomba kupata uzoefu wenu kuhusu hii Hazina Saccos Tanzania