SoC02 Hazina ya Kilimo

SoC02 Hazina ya Kilimo

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Jul 31, 2022
Posts
6
Reaction score
3
Mimi Si duni si dhaifu ni mwingi wa suluhu jamii yangu niamini, Mwenyezi Mungu si dhalimu kukuweka karibu na mimi mwanadamu amini, Niwe kwako kwanza, wanyama nchini, ndege angani Kitambaacho juu nchini, chenye uhai hata majani, miche kondeni chakula chanzo ni mimi.

Sikupi maono mapya kukomboa wakati jamii yangu, wewe wajua si siri; mimi ukombozi dhidi ya umaskini narudishia Amani familia, kaya, jamii hata Dunia.
Natumainisha wanyonge, ongezea mapato nchi yangu, tokomeza hali duni! umaskini.

sikulazimishi bali nakukumbusha;Mimi kilimo mhimili jamii shtuka.

Siombi Unikumbuke! Ila kumbuka
Mwenyezi Mungu aliowapenda aliwapatia ardhi kuimiliki, kuilima na nguvu hakuwanyima.

Abramu! Pale Kaanani, utajiri alipatiwa Upande' kaskazini, kusini, mashariki, magharibi katika nchi yote kwa marefu na mapana nchi alibarikiwa na ahadi alitimiziwa.

Joshua! ng’ambo ya Yordani, upande wa mawio ya jua na watu wake wote ndivyo alivyowaapia raha, Kuimiliki na kuitawala nchi yenye maziwa na asali BWANA hakuwazuilia.

kupitia mimi wapata chakula, hata yeye mwaweza kumjaribu mwingi wa rehema na fadhili.

Alisema “ Leteni zaka kamili ghalani wala, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu mkanijaribu kwa kwa njia hiyo, asema Bwana wa Majeshi: mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni na kuwamwagieni Baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha au la''. Asiyesahau Mwenyezi Mungu akumbushwe, Amin Utajiri awarithisha.

Kilimo ni asili yako jamii, kuendeleza urithi wa utajiri Mwenyezi Mungu alokuwekea. Basi mwambieni ye’asili wa Baraka hizi.

Mvua wakati wa masika, akupe manyunyu na kunyeshea mvua katika ardhi, afanyaye umeme ngurumo za radi angani tujue hajasahau nchi kuinyeshea na ikamea mazao ya kondeni, sawa na uzuri wa Baraka zake.

Asili yako yategemea kilimo! kabla ya kuwepo mimea, majani miche mvua kondeni.

Aliona haikupaswa uwepo bila hivyo kuilima na kuimiliki hiyo ardhi.
alipokuinyeshea mvua uso wote wa ardhi, ndipo ilistahili kukufanya kuwa nafsi hai.

Bustani kukuwekea ndani yake upande wa mashariki wa edeni kuilima na kuitunza. Ni utajiri aliokupatia, Mwenyezi Mungu hakukosea kwa maarifa na akili riziki alikuandalia.

Rudisha Imani, kumbuka nilikuwa nawe tangu mwanzo wa asili yako
Niko palepale sijabadilika, sijahama kilimo, Ulibarikiwa ukapewa utashi wa kuilima na kuitunza nchi, ikiwa nitabaki kuwa muhimili wako niamini kuitajirisha nchi na mazao kukupatia tuikomboe ulimwengu jamii yangu fahamu rudisha.

Si mnyonge kilimo mimi kukukumbusha hii asili, kabla haujapata akili na kwenda mbali, ilikupasa kutuliza akili hasa ulipojaza maarifa nayo akili.

tulia kilimo ni dili hasa ukitumia akili,
tulia itafakari kauli “ kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo kwayo ulitwaliwa” si kwa ukali kwa kauli hii bali maarifa ulirithishwa kuweka akilini.

Ikumbuke asili, ikumbuke ardhi iliyokimya, imeficha utajairi kwa maarifa fikiri, Mi’ na wewe tu ukombozi kwa jamii na hii amini kupitia asili.
Idumishe hazina hii wewe wajua kwa Imani, maarifa na akili, Ardhi imekufichia madini jipe ujasiri kupata utajiri kwa nguvu na uthubutu.

Maarifa darasani wapatiwa ni mema kufikiria na kuboresha hiyo teknolojia na Kilimo tija kukupatia.

Furaha ya pamoja ni kilimo na jamii kukua pamoja, kiakili ulivyoendelea chukua elimu weka kipaumbele ulimwengu taushangaza.

Mwanzo ulianza pale bustanini; yapasa ulimwengu uutambulishe lengo la kilimo ni kukubariki na ukombozi kwa dunia, Nasaha nakupatia, kilimo ni urithi na ukombozi ulimwenguni.

Sikutishi na dhoruba, la! Taabu wajionea kilimo na jamii kwa pamoja ni utajiri kwa dunia. Sikujaribu kwa maneno, nakukumbusha wekeza maarifa; Ubunifu pambania, elimu ulojipatia tunza yako mazingira kilimo kukilinda.

Elimu tumia; boresha yako maarifa nguvu nazo ulijaliwa tumia chako kilimo njia sahihi pitia.

Je si yote utakayo katika siku, Baraka na utajiri juu ya nchi? Je si asili pekee ndio ikupayo ardhi wa kuendeleza utajiri?

Je si urithi wa pekee waachia vizazi kutumia akili na maarifa kuendeleza utajiri kwa kilimo juu ya nchi? Je si fahari kwa jamii, taifa hata dunia kutambulisha kilimo kuwa ngao na rasilimali chachu kwa uchumi?

Kilimo si ubatili! kilimo ni akili; asili ya utajiri. Wekeza maarifa, hamasisha jamii kutumia maarifa kuikuza Nyanja hii. Watalaamu elimisha, kilimo ni mfariji kwa utu na uadilifu
Kemea hofu, acha dhana potufu kilimo kigezo cha umasikini kataa.

Kilimo nalia juu ya ukatili, uoto asilia unachofanyiwa kinyume na asili.

Ikumbuke asili, majira, nyakati mazingira vyote vyalia dhidi ya ukatili.
Ikumbuke asili, uangalie kwa usahihi kutunza hichi chakupa utajiri.

Wapaswa kumbushwa, ardhi, mimea,majani na miche kondeni vyakulilia. Mvua angani umande milimani chemchem mabondeni ukomo vyafikia.

Nitoapo wito kwako japo thamini mazingira, Mazao ulimayo, mifugo ufugayo mali shambani mwako ijafurika utajiri ni wako.

Nitunze nikutunze unitunzapo! si rafiki wa uharibifu mazingira, asili yangu ijapo haribika njaa tafurika.

Utunzaji Mazingira ni rafiki wa rafiki zangu hilo wajua! Nakuweka mbali na utumwa, vita njaa na ukimbizi hilo watambua.

Ukimbizi, machafuko, magonjwa pamoja na vifo si sifa ya mahali nilipo tambua! Nilipo natambulisha maendeleo, nakimbiliwa na wenye hekima akili kutunza vizazi vijavyo.

Mwenyezi Mungu wa ukuu na utukufu aliwapa maono aliowapenda hata wakuu wa mataifa kusema “tupate wapi mtu kama huyu, Mwenye Roho ya Mungu ndani yake” walipohitajika kuhifadhi chakula kwa miaka 7 yote ya njaa.

Nilipo kilimo jamii yanifurahia kwa kutokomeza njaa na umasiki uliokithiri
Kilimo ni uzuri juu ya nchi, chameta meta kwa kupendezesha angani.
Kilimo ni fahari kitoapo mavuno tele, jamii kushangilia watoto kufurahia wayatoapo mazao shambani.

Nguvu zao fahari yao watoapo chakula shambani, nyumbani na karama kufanyika kwa sherehe za mavuno na misimu mipya juu ya nchi.

Kilimo chasitawisha nafsi, familia kaya kwa kaya. Jua lichwapo laipongeza ardhi kwa muonekano wa kupendeza majani hata maua juu ya nchi.
Lizamapo jua lasisimusha kitovu cha ardhi, mimea kuvuma, majani kumetameta kwa machezo na utulivu.
Jioni ni wasaha kupatiana baada ya dhiki faraja nidhanu ililindwa, historia za kujenga tumaini nazo kuendelezwa, nafsi kufundishwa kilimo ndimo ilipo hazina Yako.

kijaporudisha mavuno tele! Wazee nao watoto wavutiwa nayo matokeo
Kilimo tumaini la kesho, furaha ya macho leo na ukombozi dhidi ya umasikini milele.

Kilimo ki nguvu mwilini, hazina ya maendeleo kwa taifa na urithi wa vizazi vijavyo.

Kilimo chafaa kimbilia.
kilimo kilipo ni uhai.
kilimo kilipo ni ustawi.
Imarisha ujasiri! wekeza kwa kutekeleza.
AMKA!!
255148692.jpg
1081602200.jpg
1720100790.jpg
1264842091.jpg
695105298.jpg
962119459.jpg
 
Upvote 12
Back
Top Bottom