Hazina ya Mzee Kissinger iliyoambatanishwa na maktaba ya Mohamed Said

Hazina ya Mzee Kissinger iliyoambatanishwa na maktaba ya Mohamed Said

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
HAZINA YA MZEE KISSINGER KATIKA MAKTABA YA MOHAMED SAID

Kama waandishi wa Wasifu wa Julius Nyerere wasingesema kuwa Maktaba yangu ni katika maktaba tatu bora walizoziona wakati wanatafiti maisha ya Baba wa Taifa, labda nisingejua thamani ya hii Maktaba.

Leo nimetembelewa na mwandishi chipukizi anaenyanyukia, muhitimu wa Chuo Kikuu Cha Kiislam, Mbale Uganda, Hafidh Kido.

Tumefanya mahojiano ya historia ya magazeti Tanganyika na katika mazungumzo yetu nikamweleza Hafidh kuwa lazima azungumze na mwalimu wangu Mzee Kissinger.

Tumepata fursa ya kuwakumbuka waandishi wa mwanzo Waafrika waliomiliki magazeti yao wenyewe na wao pia ndiyo wakawa wahariri wa magazeti hayo kama Erica Fiah (Kwetu), Ramadhani Mashado Plantan, (Dunia, Zuhra) na wale waliokuja baada yao na kufanya kazi katika magazeti kama waandishi, Robert Makange na Rashid Kheri Baghdeleh (Mwafrika), Julius Nyerere (Sauti ya TANU).

Nimemweleza pia hadithi za kusisimua nilizosoma nikiwa mdogo zilizokuwa zikiandikwa na Omari Chambati katika magazeti ya Baraza, na mashairi ndani ya gazeti la Mamboleo yaliyokuwa yakichapwa na Community Development Department na nikamweleza propaganda ndani ya moja ya magazeti haya hadithi katika picha za kuchora ya ‘’Rita na Makomunisti,’’ iliyokuwa ikimuonyesha Rita mwanamke mrembo aliyekuwa akipambana na Wakomunisti.

Omari Chambati naamini ndiye mwandishi wa kwanza Tanganyika kuandikia hadithi za kutisha.

Nakumbuka hadithi yake moja, ‘’Mlonji.’’

Mlonji alikuwa mtu aliyekufa akawa anafufuka usiku anaingia mjini na kuua watu na kisu chake kirefu.

Hadithi hii ilikuwa hainipiti kila wiki nikiipenda lakini ikinitisha.

Kisa hiki kilipendwa na wasomaji wengi sana.

Katika utoto wangu wa kuanza kujifunza kusoma niliwachukia wakomunisti hata kabla sijajua nini Ukomunisti na nikampenda msichana mrembo Rita.

Ikanijia kuwa nimuonyeshe baadhi ya hazina niliyorithishwa na mwalimu wangu Mzee Kissinger.

Jinsi Hafidh alivyostuka na kuchukuliwa na kile nilichokiweka mikononi mwake sikuweza kujizuia ila nikamuomba nimpige picha chache wakati akiwa katika mshangao kwa yale yaliyokuwa yakimfungukia machoni pake.

Hii ndiyo hazina ya Mzee Kissinger iliyo ndani ya Maktaba yangu.

20200720_172257.jpg
 
Back
Top Bottom