Hebatitis b confusion

mumewanguu

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2018
Posts
261
Reaction score
259
Nina ndugu yangu alienda pima akakutwa yupo hebatitis b positive, doctor akamwambia kua hatakaa apone,akaanza dozi akatumia ndani ya mwaka mzima ,juz kaenda kuchukua dawa watu wa ctc wanamhoji kwann haponi na wenzie wanapona,Sasa tushike lipi huu ugonjwa unapona au hauponi? msaada wataalam mliopo humu
 
Kuhusu Hepatitis B kuwa positive inategemea na kipimo kipi vinginevo nikuambie tu kuwa hepatitis b kuna vipimo vingi na ili mtu aanzishiwe dawa ni lazima atapima si chini ya vipimo vitatu ama zaidi ndipo daktari afikie uamuzi wa kusema anza dawa .. nakupa home work nisaidia hili huyo ndugu yako alipima kipi kati ya hivi Hepatits B surface Antigen, Hepatitis B surface Antibody, Hepatitis B viral Load quantitative ama hepatitis B core Antibody ama Hepatitis B e Antigen,
 
Ni ma-dokta mzuri? Angalia sana hospital za Bongo zina ma-dr vilaza kuliko! Huo ugonjwa unaweza kutiba lakini wakati mwingine unaweza usitibike. La muhimu apime na kutibiwa sehemu zenye uhakika. Na akimwona dr zaidi ya mmoja itakuwa vizuri zaidi.
 
Hepatitis b surface antigen
 
Unapona ila kwa tiba mbadala na kubadilisha diet, mbona kuna rafiki yangu na bro wsngu wamepona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…