Waraka dhaifu kama huo hauwezi kuwa umetokana na kikundi chochote ambacho ni makini, waraka wa siri wewe umeupata wapi?
Hizo simple minded zako zitatugharimu sana kama watanzania.
Waraka huo utakuwa umetolewa na kundi linalohangaika kurudi madarakani kwa kutumia familia badala ya chama, na ni namna ya kutafuta kuonewa huruma na wapiga kura, hakuna kitu cha maana hapo.
Watanzania kama tulivyo tuko sensitive sana kwenye mambo ya dini bila hata ya utafiti wa kina mtu akiambiwa kwamba hili suala linatokana na itikadi fulani bila kujali kwamba ni uzushi au la mtu anaamua kufanya ushabiki.
Binafsi mimi si mrahisi hivyo na ubaguzi wowote unanikera katika kiwango kwamba hata msamiati wa kuelezea kero hii umenipita kushoto ila nasisitiza kwamba ubaguzi wa namna yoyote tusiukubali. Watu wana malengo ya kisiasa kuhusu hili hivyo walio huru kufikiri waliangalie hili kwa makini.