HEBU CHEKA UONGEZE UMRI WAKO ...KUISHI......

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
MBUNGE ULAYA: Mheshimiwa Spika napenda kujua ni lini serikali itakarabati barabara ya Adam's court?

WAZIRI: Mheshimiwa Spika napenda kumhakikishia mbunge kuwa barabara hiyo itajengwa katika kipindi cha mwaka ujao wa fedha na kufikia October 1 mwakani itakua imekamilika?

MBUNGE BONGO: Mheshimiwa Spika ni lini serikali itajenga barabara ya Tabora Mbeya kupitia Chunya?

WAZIRI: Mheshimiwa Spika awali ya yote nimpongeze mheshimiwa mbunge aliyeuliza swali. Serikali inatambua umuhimu wa barabara hii hasa kuunganisha watu wa mikoa ya magharibi na

nyanda za juu kusini. Barabara hii itachochea kasi ya maendeleo hasa usafirishaji wa mazao ya chakula na biashara katika maeneo haya mawili. Pia itaongeza wigo wa ajira kwa vijana na

kuwezesha usafirishaji wa vipuri kwa ajili ya uanzishaji wa viwanda. Barabara hii ilibuniwa mwaka 1922 na serikali ya wajerumani kwa ajili ya kusafirisha vibarua wa mashamba ya tumbaku Tabora

kutoka Mbeya. Mwaka 2015 serikali ilikarabati barabara hiyo kwa kiwango cha Changarawe, na hivyo basi kwa kutambua umuhimu wa barabara hiyo serikali itaendelea kuikarabati mara kwa mara na ikiwezekana kuijenga kwa kiwango cha lami. Asante. (makofi pwapwapwa)!
 
Swali halijajibiwa hapo, bali katoa historia ya barabara hiyo!
Ni Kweli halijajibiwa na Mheshimiwa Waziri Muhusika bali ameeleza Historia ya barabara pasipo na kujibu swali alilo ulizwa na muheshimiwa Mbunge. bungeni ni malumbano majibu ya uhakika hakuna.
 
Mbunge mzalendo [emoji3][emoji3][emoji3]
 
MBUNGE ULAYA: Mheshimiwa Spika napenda kujua ni lini serikali itakarabati barabara ya Adam's court?

WAZIRI: Mheshimiwa Spika napenda kumhakikishia mbunge kuwa barabara hiyo itajengwa katika kipindi cha mwaka ujao wa fedha na kufikia October 1 mwakani itakua imekamilika?

MBUNGE BONGO: Mheshimiwa Spika ni lini serikali itajenga barabara ya Tabora Mbeya kupitia Chunya?

WAZIRI: Mheshimiwa Spika awali ya yote nimpongeze mheshimiwa mbunge aliyeuliza swali. Serikali inatambua umuhimu wa barabara hii hasa kuunganisha watu wa mikoa ya magharibi na

nyanda za juu kusini. Barabara hii itachochea kasi ya maendeleo hasa usafirishaji wa mazao ya chakula na biashara katika maeneo haya mawili. Pia itaongeza wigo wa ajira kwa vijana na

kuwezesha usafirishaji wa vipuri kwa ajili ya uanzishaji wa viwanda. Barabara hii ilibuniwa mwaka 1922 na serikali ya wajerumani kwa ajili ya kusafirisha vibarua wa mashamba ya tumbaku Tabora

kutoka Mbeya. Mwaka 2015 serikali ilikarabati barabara hiyo kwa kiwango cha Changarawe, na hivyo basi kwa kutambua umuhimu wa barabara hiyo serikali itaendelea kuikarabati mara kwa mara na ikiwezekana kuijenga kwa kiwango cha lami. Asante. (makofi pwapwapwa)!
Mwaka 1922 kulikuwa na mjerumani gani wakati nchi ipo mikononi mwa waingereza toka mwaka 1919
 
Back
Top Bottom