Hebu lete "top 3" ya mechi bora za fainali UCL kuanzia mwaka 2000 na kuendelea

kombaME

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2015
Posts
2,115
Reaction score
2,818
Kwa upande wangu

1.2005, Ac milan vs Liverpoo, dk 90 3-3 then Liverpool akawa bingwa kwa matuta

2.2006, Barcelona Vs Arsenal, dk 90 2-1, Arsenal anakufa kikatili sana, enzi hizo arsenal ni ya moto, niwaambie tu wadogo zangu, Arsenal mnayoiona sio hii.

3.2008, Man u Vs Chelsea, dk 90 1-1, Matuta man u bingwa, Penalty 5 zilisha kwa timu zote, Terry anateleza anakosa penalty, ndo basi tena.

Vipi kwa upande wako?
 
Hii ya john Terry ilivuma Sana hasa alipo mnyandua mke wa mchezaji wenzake I hope ni mke WA J.Cole

UCL 2005 ya Liverpool na AC Milan is the best Kwangu
 
Nadhani ule mpira asili ndo ulikuwa unaishia hapo, kila nikijaribu kuangalia soka siku hizi, sielewi elewi tena kama siku hizo zilizopita.

Naona kama kabumbu linajifia kama zilivyokufa ndondi za level ya akina Tyson.

Yaani ungeanzia mwaka 1998 WC, au hata nyuma ya hapo, fainali ya Egypt na Bafanabafana 1996 kama nakumbuka vizuri. Soka safi, vipaji lukuki, sio soka la kutawaliwa na CR7 na Messi kwa miaka 10 kama wako peke yao
 
Yawezekana wewe ndo umezeeka bro,
 
1. Inter Milan vs AC Milan (2002/3) mechi zote mbili za semi final
2. Deportivo La Coruna vs AC Milan (2003/4) hii mechi ya pili Milan anapigwa 4-0 wakati mechi ya kwanza alishinda 4-1
3. Hapa ni 2013 Bayern Munich vs Barcelona (7-0 agg)

Dah nimewakumbuka kina Walter Pandiani, Dado Prso, John Carew, Morientes, Ben McCarthy, Jan Koller, Milan Baros etc
 
Yawezekana wewe ndo umezeeka bro,
Ni sawa pia, lakini wewe kama uliliona lile kabumbu la kipindi hicho, ukiangalia timu moja unaona imesheheni kila idara, soka safi. Ipi timu unayodhani imetimia kwa sasa? Atletico? PSG? Juventus? Borussia Dortmund? Ajax? Alcantara? Sporting Lisbon? Ipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…