Hebu mwangalieni huyu lecturer wa udom

Hebu mwangalieni huyu lecturer wa udom

UDOM SR

Member
Joined
Jan 25, 2014
Posts
47
Reaction score
26
Hivi huku vyuoni hakuna mechanism ya kuwafuatilia hawa walimu ufundishaji wao, au ndio wakishaajiliwa imetoka wanaendelea kufundisha wanavyojua wao na hakuna cross-checking maana kuna walimu hapa Udom ni majanga, Nilitaka kutoa details za huyu lecturer lakini nimeona nisubiri nimalize semester kwanza maana anaweza kugundua kuwa ni mimi ndio niliouza file lake halafu akanila kichwa. ila ndio tunamalizana nae semester hii. kwa hiyo vuteni subira.
 
Kwani hapo hakuna assesment ya walimu kila mwisho wa mwaka mtoe ya kwenu?
 
Tatizo ajira za hapo magumashi hawaangalii ujuzi au uwezo wa m2.
 
Kiongozi hakuna dhambi mbaya kama uoga.Mi nadhani jambo la msingi sikukichafua chuo chako.Mfuate academic adviser wako mwambie tatizo lako atakushauri nini chakufanya kutokana na somo analofundisha unayemlaumu.Huku kwenye majukwaa ni tofauti na kwenye academic institution.Unaweza ukasympathise na sisi huku mwisho wa siku ukaumia mwenyewe.Mara ya mwisho ulipoandika uliregret sasa leo umerudi jitafakari alafu uchukue hatua huko hakuna siasa mimi ziliniponza.
 
nasikia hapo kuna matatizo mengi sana na ubabaishaji wa kutosha
 
Hivi huku vyuoni hakuna mechanism ya kuwafuatilia hawa walimu ufundishaji wao, au ndio wakishaajiliwa imetoka wanaendelea kufundisha wanavyojua wao na hakuna cross-checking maana kuna walimu hapa Udom ni majanga, Nilitaka kutoa details za huyu lecturer lakini nimeona nisubiri nimalize semester kwanza maana anaweza kugundua kuwa ni mimi ndio niliouza file lake halafu akanila kichwa. ila ndio tunamalizana nae semester hii. kwa hiyo vuteni subira.

Unaloweza kufanya ni kuishawishi serikali ya wanachuo mu introduce assessment ya lecturers bila kuweka jina kwenye assessment sheet. lakini iwe katika kumsaidia lecturer aboreshe "ufundishaji" na sio katika mtindo wa majungu na mud slinging.

wa Tz tuna hulka au mila ya kuogopana - wenzetu weupe tokea shule ya msingi hadi vyuo vikuu wanaandama na kugomea walimu wabovu na sio kwa vile wamepewa chakula kibovu!! huo ndo utamaduni wao - mwanafunzi anaweza mwambia mwalimu kuwa huo sio ukweli na wakabishana hadi mmoja wao akaukubali ukweli.
 
Kiongozi hakuna dhambi mbaya kama uoga.Mi nadhani jambo la msingi sikukichafua chuo chako.Mfuate academic adviser wako mwambie tatizo lako atakushauri nini chakufanya kutokana na somo analofundisha unayemlaumu.Huku kwenye majukwaa ni tofauti na kwenye academic institution.Unaweza ukasympathise na sisi huku mwisho wa siku ukaumia mwenyewe.Mara ya mwisho ulipoandika uliregret sasa leo umerudi jitafakari alafu uchukue hatua huko hakuna siasa mimi ziliniponza.

huyu mleta mada anadhihirisha aina ya wasomi tulionao nchi hii.
maskini taifa linaangamia
 
Tatizo wabongo mnapenda kufundishwa kama shule ya msingi wakati mpo chuo, nimefundishwa na mhindi mmoja, anatupa course outline kazi kwako kukomaa, ukizoea vya dezo lazima utaona baadhi ya wahadhiri hawafai kumbe hufai wewe
 
sasa kama course outline ndio kusoma basi tusingeenda chuo kufundishwa tungepewa course tujisomee tuu majumbani kwetu, chuo tunafuata ujuzi na sio kukariri kwa ajili ya mtihani... kuwa muelewa kijana.
 
Subiri mpaka graduation ipite jinalako liwe kwenye kale ka kitabu na uchukue cheti ndio uandike. La sivyo ARIS itakacho kufanyia hutakaa usahau
 
Kweli Udom nimesoma pale kun matatizo ya mfumo. Watu wanapeana vyeo kama njugu, udini, ukabila na ukanda ndizo nguzo kuu za chuo cha Udom. Unaweza dhani hakiko Tz labda kiko S sudan. Inakera lakini fuata yaliyo kupeleka kisha chukua cheti sepa. Ukimfuatilia bata huta kula nyama yake vivyo hivyo kwa Udom. Kama ingekuwa rahisi kuhama chuo kama ilivyo kwa elimu ya sekondari mimi ningehama Udom, ila nilikomaa nikahitimu kwa sasa naendelea na mishe mishe zangu. Serikali ndio inakiua Udom.
 
Ndugu piga msuli, hata lecture akiwa mbaya vipi ukiondika hapo huondoki nae utaondoka peke yako na skill uliyokua nayo tu
 
Tatizo wabongo mnapenda kufundishwa kama shule ya msingi wakati mpo chuo, nimefundishwa na mhindi mmoja, anatupa course outline kazi kwako kukomaa, ukizoea vya dezo lazima utaona baadhi ya wahadhiri hawafai kumbe hufai wewe

Ulikuwa unasoma course gani? Pamoja na swali hili sidhani kama kuna course unaweza kujifunza mwenyewe bila facilitator, mmhh huyo muhindi wako nae hakufunzwa hivyo
 
Kaka usibishane na mtu asie jitambua. Huyo anaishi kwa kukalili wewe kama ulifundishwa na Mhindi anae kupa Course outline pekee na kukuambia ujitafutie unataka kila mwanachuo afundishwe hivyo? Kwa anaesomea udaktari je? Uhandisi je? Fikri kabla ya kusema, njia ambayo wahadhiri wanapaswa kuitumia ni "modified lecture method inayo mpa uhuru mwanachuo kuuliza swali na hata kuchangia hoja". Kwa wahadhiri waliopatikana kimagumashi hawapendi kuulizwa maswali, wanahofu kitanuka kuwa ni mamluki wa elimu. Vyuo vingi vya sirikali vina watu wa namna hiyo hasa Udom. Kuna mhadhiri mmoja aliwahi kutufundisha FE 200 huyo dada alikuwa mtupu kwa kichwa, alikuwa anasoma kama anavyosoma gazeti la Udaku, hakuna hata kupunguza wala kuongeza point, pia hapendi umuulize swali anachukia. Sasa utapata picha ya baadhi ya wahadhiri wetu.
 
Tatizo wabongo mnapenda kufundishwa kama shule ya msingi wakati mpo chuo, nimefundishwa na mhindi mmoja, anatupa course outline kazi kwako kukomaa, ukizoea vya dezo lazima utaona baadhi ya wahadhiri hawafai kumbe hufai wewe

kumbe wewe umefundishwa kwa kukariri ?? ndio maana uko hivyo wala sio kosa lako
 
Hivi huku vyuoni hakuna mechanism ya kuwafuatilia hawa walimu ufundishaji wao, au ndio wakishaajiliwa imetoka wanaendelea kufundisha wanavyojua wao na hakuna cross-checking maana kuna walimu hapa Udom ni majanga, Nilitaka kutoa details za huyu lecturer lakini nimeona nisubiri nimalize semester kwanza maana anaweza kugundua kuwa ni mimi ndio niliouza file lake halafu akanila kichwa. ila ndio tunamalizana nae semester hii. kwa hiyo vuteni subira.

Unasema tumwangalie, yupo wapi mbona mi simwoni
 
Back
Top Bottom