Wakuu,
Wazee wa mashati ya kijani wameishiwa, hawana mapya, ndo maana kujihami wamwekimbilia kuwaleta wanafunzi katika kampeni za uchaguzi. Wanafunzi ambao hata maana ya uchaguzi hawajaijua, wanafunzi ambao sifa ya raia hawaijui, hii ndo CCM, kujaza mapengo kuuonyesha umma wa ndani na nje kuwa wanakubalika. Ili kazi ya KUCHAKACHUA kura isiwe ngumu na ikose upinzani!!!
CCM imelaaniwa kwa maovu na machafu yote waliyotufanyia kwa miaka takribani 50 toka uhuru!! Yanawarudia ndo maana hawawezi kubadili watu otherwise...
Nasema kuchakachua kura ni dhambi yao, lakini tukikataa kuwapa ridhaa hata uchakachuzi utashindikana, maana nina uhakika watachanganya madesa!!! Dawa ni kuhamasisha wooooooooooote ndani ya kaya zetu, tukapige kura kwa kuleta mabadiliko; hawa tumewazoea...
Ukianzia ndani mwako changes will certainly come to TZ!!