Dr wa Manesi
JF-Expert Member
- Aug 19, 2024
- 997
- 1,220
Naanza Mimi. Imenitokea mara mbili;
1. Nilipigana kabisa na msichana flani tukiwa shule ya msingi (darasa la 6). Alinichongea kwa mwalimu nami nikamtafuta baadae na kuzibuana nae vibao; mitama miwili na vibao vitatu swaaafi kabisa vikamkuta. Nikaripotiwa tena na viranja nikaadhibiwa tena vikali. Uadui kati yangu na yule Binti ukaendelea zaidi.....hatusalimiani Wala hatuongei. Ikafika likizo. Ndani ya likizo nikajikuta kama anatokeatokea hivii akilini siku Moja Moja (mtakumbuka kipindi kile (90s) tulikuwa tunasoma tukiwa wakubwa).
Tukafungua shule. Siku Moja nikambamba akiwa peke yake nikamsalimia kwa amani tu tofauti na matarajio yake. Ile kitu ikamtabasamusha na kuanzia hapo tukawa tutaongea. Ilichelewa, mara huyo akawa partner wangu yule dada. Aisee penzi lililoibuka hapo, sitokuja kusahau.......tulipendana mpaka tunamaliza la saba, tukaendelea kupendana mpaka tumemaliza kidato Cha nne. Tumeendelea kupendana mpaka Leo (km marafiki wa kawaida kwa Sasa; nimeona, ameolewa)
2. Nikiwa chuo, siku Moja niligombana na mdada flani. Kisa ni Cha kipuuzi kabisa. Alihisi nimemgusa na kumsukuma mlangoni wakati tunatoka lecture theatre tunakimbilia kupumzikia nje. Akanitolea mbovu nami nitafanya hivyo pia. Ikawa si njema kwa 'social status' yetu kwakweli. Nikakaa kama wiki tatu hivi nikiwa sisalimiwi nae nami simsalimii. Mwishowe nikaona mambo yasiende hivi. Nikamtafuta, neno la kwanza nililomwambia baada ya kusalimia ni kuwa, 'unajua mi nakupenda sana?!'. Baada ya purukishani za hapa na pale mwishowe tukawa wapenzi wazuri kuanzia mwaka wa kwanza muhula wa pili Hadi tunamaliza chuo. Tulishibana na tulienjoy haswaa.....Kila mmoja alijua kuwa tunaenjoy.
Twende na chako......