Hebu tujadili mtizamo huu wa kitofauti katika biashara:

Mr.genius

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2012
Posts
1,374
Reaction score
1,201
Habari zenu wakuu na heri ya mwaka mpya, wakati tukiendelea kuukaribisha mwaka mpya hebu tuukaribishe na mtizamo huu katika biashara, kwamana kwamba kuna ukweli wowote katika mitizamo hii ama la..
Napenda kujua na natupanuane mawazo katika hili 1.UKABILLA NA UTAIFA KATIKA MAFANIKIO YA KIBIASHARA
Nachopenda kufaham hapa ni je nikweli kukua kwa biashara katika ustawi mzuri na wakuridhisha kwa namna moja au nyingine inategemea na ni mtu wa kabila gani au taifa gani anaeisimamia biashara hiyo? Kwa mfano kwa hapa kwetu tanzania kuna kabila la wachaga hawa wanacfka sn kwa kufanya biashara na ndio wanaoongoza kwa kuwa na maduka na mambo yanayohusianan na biashara hapa nchini kwetu, sasa nataka kujua inamana katika nadharia ya biashara jambo hili linamchango gani? Mana unaweza ukakuta mfano mtu anatafuta mtu wa kufanya biashara labda dukani kwake ama sehemu fulan bac priority ya kwanz a anamtafuta mchaga akiaminii ndo wanaweza sana biashara vizuri zaidi na ikawa na mafanikio
Tukija la utaifa utaona moja kat ya wanaoongaza kuwa na maduka na biashara kubwa kubwa ni waarabu na wahindi inamana hawa wenzetu wamezaliwa kufanya biashara tu na ni kweli wafanyapo biashara lazma litoke
2.KIPAJI
La pili pia napenda kufaham suala la kipajii binafsi cha mtu kufanya biashara, mana utackia wakati mwingine mtu akisema "aah! Jamaa huyu anakipaji cha kufanya biashara bwana yani akishika yeye duka mambo yanakwenda" sasa je, kama ilivyokuna kipaji mwingne cha kuimba muziki, mwingine kutunga nyimbo n.k na mwingine anakipaji cha kufanya biashara? Kwa sehemu nmeshuhudia hili watu unawakuta wanasema dah! Duka lile wakati anauza fulan halikua na wateja sana lakini alipokuja fulani dah bidhaaa znatoka kweli na wateja wanajaa sna kwel jamaa anamkono wa biashara(anakipaji cha biashara) je kipaji cha kufanya biashara kweli hili swala lipo kwenye kufanya biashara na linafanya kaz kweli kwa ustawi na kukua kwa biashara flani?? Nawasilisha..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…