Hebu tujikumbushe enzi za Tambaza na Azania kabla Tambaza kubadilishwa kuwa high school

ommytk

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Posts
520
Reaction score
1,143
Kwa wenye kumbukumbu hizi shule kulikuwa na mchaka mchaka hatari tambaza hizo hizo kuna mtu anaitwa puza mchafu marehemu alikuwa mth na nusu yaani stand faya pale ilikuwa uwanja vita kila siku daaah mpk tambaza ikabadlshwa kuwa high school ikatulia kidogo
 
Daaa mm ni mmojawapo wa wanafunzi wa tambaza 94 nikiwa form 2.Inanikumbusha mbali sana hadi tukapewa suspension mwaka mzima kisha tukahamishiwa mikoani,noma sana mhenga mwenzangu.
 
Na yule mzee wa jembe ni jembe akachapwa viboko kwa kuiba Abbott physics na Mwl. Mchwampaka 🤣🤣🤣🤣
 
Na yule mzee wa jembe ni jembe akachapwa viboko kwa kuiba Abbott physics na Mwl. Mchwampaka [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Mwl Mchwampaka ni wa Geography ilikuaje alitoa adhabu?
Kuna siku tulitembeza kipigo kwa makonda kutoka Muhimbili mpaka fire baada ya mwanafunzi mmoja kufariki Buza huko,
Azaboi taifa kubwa
 
Kwa wenye kumbukumbu hizi shule kulikuwa na mchaka mchaka hatari tambaza hizo hizo kuna mtu anaitwa puza mchafu marehemu alikuwa mth na nusu yaani stand faya pale ilikuwa uwanja vita kila siku daaah mpk tambaza ikabadlshwa kuwa high school ikatulia kidogo
Na hakuna Mwanafunzi aliyekuwa akisoma Azania na Tambaza Kipindi hiko asiyekuwa Mtukutu ( Naughty ) lakini ni Mwerevu ( Brainiac ) sana Darasani.

Mitoto mingi ya Siku hizi ni legelege ( utopolo ), mivivu, haipendi Kusoma, inadeka na Kudekezwa mno na Wazazi wao halafu ni Mingumbaru ( Mijinga ) na Mipopoma ( Mipumbavu ) zaidi.
 
Marehemu Puza alikuwa mtabe haswa ila pia alikuwa na matatizo ya akili, jamaa alijiua kutokana na msongo wa mawazo na sonona (depression).

Ukizungumzia Tambaza na Azania usisahau watoto wazuri wa Jangwani kisutu na zanaki enzi hizooo.
 
Sasa wakati tambaza inasambaratishwa kuna wale waliletwa Iyunga technical Mbeya walisafiri kwa treni ya Tazara du kumbe Mbeya nako kulikuwa na watoto wamevurugwa kutoka mbozi Chunya kyela ileje umalila watoto wababe hatari wanakula kile kitu cha moshi vijeba vimejazia muda wote ngumi mkononi vikawa vimeshajua time table ya wale wajanja wa mjini wanaingia na treni jioni ... wakaenda pale Tazara station kuwasubiri ile treni inaingia inapaki wakalakiwa kwa nderemo na vifujo watoto wa iyunga kila begi ya Tambaza ikishuka wanasachi mikate na dikodiko zingine pamba wanatest wanajisevia ukileta uzuri unachanjwa na wembe alafu pale pembeni wale wababe wenyewe wa shule wametulia wamevaa mizura wanakula moshi..... aise ilikuwa patashika kuna watoto wa tambaza walikuwa na roho nyepesi walirudia palepale station.
 
My School
school_logo.png
 
Hahaha umeua sana

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom