MakinikiA
JF-Expert Member
- Jun 7, 2017
- 5,104
- 6,827
Sergei Surovikin: Mfahamu jenerali mpya wa Urusi maarufu kwa ukatili wake
Rais wa Urusi Vladmir Putin alimpatia kazi mmojawapo ya watu wake maarufu katika mstari wa mbele wa vita nchini Ukraine wikendi hii.
Jenerali wa jeshi la nchi kavu Sergei Surovikin aliteuliwa siku ya Jumamosi kuwa kamanda mpya wa jeshi la pamoja katika operesheni maalum inayoendelea ,kama jinsi Kremlin inavyotaja uvamizi wa taifa hilo Jirani.
Kufuatia uamuzi huo, Moscow ilitoa ujumbe kuhusu mkakati wake wa kivita baada ya kuchomeka moto na hadi kuanguka kwa daraja la Crimea Jumamosi iliopita kutokana na mlipuko wa lori ambao ulisababisha malori mengine saba ya mafuta kuungua. Ukraine haikudai kutekeleza shambulio hilo.
Siku mbili baadaye , siku ya Jumatatu , Urusi iliishambulia Kyiv na makombora baada ya miezi kadhaa bila ya kutekeleza mashambulizi katika mji huo mkuu wa Ukraine.
Putin aliita jibu la "kitendo cha kigaidi" ambacho alilaumu serikali ya Volodymyr Zelensky.
Lakini pia ilikuwa ni jibu la Putin kwa mwewe katika kambi yake, ambao wanazidi kuhangaika na hasara ya Urusi katika vita na kuongezeka kwa wito wao wa kuchukua hatua kali, kulingana na Sarah Rainsford, mwandishi wa BBC huko Ulaya Mashariki.
Maafisa wa Kremlin na watangazaji wa Televisheni ambao walikuwa wamevunjika moyo na kukata tamaa siku chache zilizopita sasa wanapongeza shambulio hili dhidi ya jirani zao, kufurahi na hata kucheza kwenye mitandao ya kijamii, huku Ukraine ikiomboleza waliokufa na uchafu kutokana na mashambulizi mengi.
Jenerali mwenye uzoefu
Surovikin anatoka Siberia, ana umri wa miaka hamsini na sita na ana uzoefu mkubwa wa kijeshi , alipigana nchini Afghnaistan, Chechnya, Tajikistan na Syria. Ana uzoefu wa ukatili ijapokuwa anaonekana nchini Urusi kuwa jasiri na asiyetaka mchezo " .
Huko Chechnya, ahadi yake ya hadharani ya "kuwaangamiza wanamgambo watatu kwa kila askari aliyekufa" ilipata sauti kubwa, kulingana na shirika la habari la Urusi TASS.
Kabla ya kuteuliwa kuwa jenerali wa jeshi mnamo Agosti 2021, Surovikin alipigana vita huko Syria.
Huko aliongoza kundi la wanajeshi wa Urusi nchini humo tangu Machi 2017 na, kulingana na TASS, alichukua udhibiti wa eneo kubwa, viungo vikuu vya usafirishaji na uwanja wa mafuta, kati ya zingine.
Jenerali Surovikin akiwa katika mkutano wakati wa vita nchini Syria
Mnamo Novemba 2017 aliteuliwa kuwa Kamanda Mkuu wa Vikosi vya Anga vya Urusi na hivyo kuwajibika kwa uharibifu wa angani wa sehemu kubwa ya jiji la Aleppo nchini Syria.
Na mwezi mmoja baadaye alitunukiwa na Putin: alipokea jina la shujaa wa Shirikisho la Urusi "kwa ujasiri na ushujaa ulioonyeshwa katika utendaji wa kazi ya kijeshi katika Jamhuri ya Kiarabu ya Syria."
Simulizi ya jenerali huyo pia inajumuisha kifo cha waandamanaji wanaounga mkono demokrasia mjini Moscow mwaka 1991 wakati wa jaribio la mapinduzi, ambapo tayari alitajwa kuwa katili.
Mwanajeshi huyo alikamatwa wakati huo, lakini Rais wa Urusi Boris Yeltsin aliamuru kuachiliwa kwake, kulingana na TASS.
Tukiangazia Ukraine
Surovikin tayari alikuwa akiongoza kundi la "Kusini" la wanajeshi nchini Ukraine tangu mwaka huu na, kwa mujibu wa Frank Gardner, Mwandishi wa Habari wa Usalama wa BBC, haijafahamika ni tofauti gani uteuzi wake utaleta.
Huko Ukraine, Urusi inakabiliwa na jeshi la kweli, lililo na vifaa na mafunzo kutoka kwa nchi za NATO, na Warusi wamekuwa wakipoteza ardhi na heshima yao.
Huko Ukraine, Urusi inakabiliwa na jeshi la kweli, lililo na vifaa na mafunzo na nchi za NATO, na Warusi wamekuwa wakipoteza ardhi na heshima.
Ikulu ya Kremlin imepoteza majenerali kadhaa waliouawa katika mstari wa mbele na wengine kufukuzwa kazi kwa kukosa uwezo.
Na wenye msimamo mkali mjini Moscow wamekuwa wakipigia kelele kuhusu mbinu kali zaidi ili kufikia lengo lao la kuitiisha Ukraine.
Tukio la daraja la Crimea lilizua wasiwasi wa Urusi katika hatua zilizopigwa katika mstari wa vita
Kumteua Surovikin kuongoza jeshi Ukraine ilikuwa "makubaliano ya Putin kwa watu wenye msimamo mkali," anasema Rainsford.
Kwa muda mrefu wametoa wito wa mashambulizi dhidi ya miundombinu ya kiraia: kufungia watu wa Ukraine katika majira ya baridi hii, ikiwa askari wao hawawezi kushindwa kwenye uwanja wa vita.
"Tutaanza lini kupigana?" alidai mpiga propaganda Vladimir Solovyov, akisema kwamba ni bora kwa Urusi kuogopwa kuliko kudhihakiwa.
Grigory Yudin wa Shule ya Moscow ya Sayansi ya Kiuchumi na Kijamii alielezea mashambulizi makubwa ya Jumatatu kama "kitendo cha kukata tamaa" kilicholenga hasa kutatua matatizo ya ndani ya Putin.
Rais wa Urusi anaonekana kukubaliana na wazo la kizungu kwamba unapaswa "kumtisha mpinzani afe" ili ajiondoe, Yudin aliandika kwenye Twitter.
Rais wa zamani wa Urusi Dmitry Medvedev, ambaye aliwahi kuonekana kama mtu aliyekuwa na mtazamo huru , ameonya kwamba mashambulizi haya ni "kipindi cha kwanza", na mengine zaidi yanakuja.
"Ni wazi kwamba vikosi vyake kwa sasa vimeenea sana katika nyanja nyingi. Iwapo Surovikin atapanga kufikiria upya na kwa kina, anaweza kuamua kuzingatia eneo moja na kutumia nguvu kubwa sana,” Gardner anachambua.