Hebu tutafakari kidogo,Watanzania tunashindwa wapi miss world?

Mrzohan

New Member
Joined
Oct 18, 2018
Posts
2
Reaction score
0
Kilele cha mashindano ya miss world kimekamilika huku Kwa africa mashariki tukifanikiwa kuwakilishwa na Uganda ambao wamefanikiwa angalau kuingia katika tano bora.

Kama Uganda wamefanikiwa kuingia tano bora...unahisi tatizo ni nini hasa tanzania tumeshindwa huku uganda wakifanikiwa?

Nimeona watu maarufu tu kama millardayo mange kimambi na watu wengine wakatoa promo kubwa tu lakini mambo hayakuwa kama ilivyo tarajiwa wewe unahisi tatizo nini hasa

Video alivyo tangazwa mshindi
https://youtu.be/tgFUelF81AQ

Elizabeth mshiriki kutoka tanzania

Mshiriki kutoka uganda

Kwani haya mashindano Yana Tija gani kwa sisi vijana wa leo?.
 
Si uzuri wa sura tu unaangaaliwa, kuna agenda ya kusaidia the disadvantaged in the society. Sujui miss wetu angejibu nini swali kama “ukiwa kama msichana na miss Tanzania 2018 utawasaidiaje waliopata mimba za utotoni”?
 
Nikikumbuka basila alivyomchamba wolper kiss zawadi ya Miss Tanzania, sipati picha binti angekanyaga top five,wolper angekoma na parachuti zake
 
Kitu pekee tunachoshinda watanzania ni Big Brother
 
Kamati yenyewe ni MASIKINI SANA
NI VIGUMU MASIKINI KUPENYA MAHALI POPOTE KATIKA DUNIA HII
Lazima uwe na strategy za beyond human thinking ili kupursue
Hii biashara tuachane nayo tu
Tu focus kwenye issues zamaendeleo ya utajiri mkubwa!
 
Si uzuri wa sura tu unaangaaliwa, kuna agenda ya kusaidia the disadvantaged in the society. Sujui miss wetu angejibu nini swali kama “ukiwa kama msichana na miss Tanzania 2018 utawasaidiaje waliopata mimba za utotoni”?
Kuunga mkono juhudi za jpm hakuna namna
 
Si uzuri wa sura tu unaangaaliwa, kuna agenda ya kusaidia the disadvantaged in the society. Sujui miss wetu angejibu nini swali kama “ukiwa kama msichana na miss Tanzania 2018 utawasaidiaje waliopata mimba za utotoni”?
Pia ule u natural, unakuta miss wetu kajivalia bonge la nywele bandia. Kwanini asinyoe tu akawa na nywele zake halisi?
 
Miss Tz aliyewakilisha vzr alikuwa Nancy Sumari tu 2005, na alikuwa simple sana but beautiful
 
Kila jambo na wakati wake!.Iko siku tutaingia hadi top 3.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…